Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao Kutoka Wizara ya Kilimo,
Chakula na Ushirika Dk.
Mshindo Msolla akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa huduma ya taarifa za
kilimo kupitia Kampuni ya simu ya mkononi ya Zantel jijini Dar es Salaam leo. Wa
pili kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasirimali Watu wa Zantel, Francis Kiaga. (Picha na Francis
Dande)
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao Wizara ya Kilimo,
Chakula na Ushirika Dk.
Mshindo Msolla akizindua huduma ya taarifa za kilimo kupitia simu za mkononi.
Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Rasirimali Watu wa Kampuni ya Zantel, Francis Kiaga. (Picha
na Francis Dande)
Na Mwanablog Wetu
KAMPUNI ya simu
za mkononi ya Zantel kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, chakula na Ushirika
pamoja na Kampuni ya Sibesonke wamezindua huduma mpya ya kutoa taarifa kuhusu
kilimo kwa kupitia simu za mkononi.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo ulifanyika katika Ofisi za Wizara ya Kilimo jijini Dar es
Salaam leo, Mkuu wa Kitengo cha Rasirimali Watu wa Zantel, Francis Kiaga amesema kuwa, wameamua kuingia ubia na Wizara hiyo ili kuwanufaisha wakulima ambao watapata
taarifa za moja kwa moja kupitia simu zao.
Kiaga amesema kuwa "kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa nchi hii watapata fursa ya kujua
zaidi kuhusu kilimo ikiwa ni pamoja na kuuliza maswali kwa kupiga *141*50# na
kujipatia taarifa juu ya utayarishaji wa shamba mpaka hatua ya kuvuna sambamba
na Ufugaji bora".
“Kupitia huduma hii ya Z-Kilimo, tunaimani
kubwa wakulima watanufaika na kujua mambo mengi kama kujua aina nzuri ya mazao
na wakati gani wa kulima zao hilo na kuju jinsi ya ufugaji bora na kudhibiti
magonjwa kama mafua ya ndege ambayo usumbua mifugo mingi hapa nchini,”
“Kwani huduma
hii imekuja wakati muafaka wa kuendeleza juhudi hizo kwani huduma hii itawasaidia
wakulima kujua upaliliaji, taarifa za usafiri, hali ya hewa, mazao, aina za
mifugo, magonjwa pamoja na sehemu ya majadiliano baina ya wakulima,”
Kiaga aliongeza kuwa huduma hiyo kwa siku 14 za mwanzo kuanzia jana ni bure na baada ya hapo itakuwa sh 20 tu Faida nyingine alisema ni kujua aina nzuri ya mazao na wakati gani wa kulima zao hilo na kudai kuwa hata katika mifugo watajua jinsi ya ufugaji bora na kudhibiti magonjwa kama mafua ya ndege ambayo usumbua mifugo mingi hapa nchini.
Kiaga aliongeza kuwa huduma hiyo kwa siku 14 za mwanzo kuanzia jana ni bure na baada ya hapo itakuwa sh 20 tu Faida nyingine alisema ni kujua aina nzuri ya mazao na wakati gani wa kulima zao hilo na kudai kuwa hata katika mifugo watajua jinsi ya ufugaji bora na kudhibiti magonjwa kama mafua ya ndege ambayo usumbua mifugo mingi hapa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Maendeleo ya Mazao nchini, Mshindo Msola alieleza kufurahishwa na huduma hiyo na kudai kuwa, itakuwa fursa nzuri kuwafungua wakulima hapa nchini na kuvuna mazao yaliyo bora zaidi tofauti na sasa.
Katika
kufanikisha wakulima wanapata elimu bora juu ya kilimo na ufugaji, Sibesonke
wao wameingia ushirikiano wa Kiteknolojia na Wizara hiyo pamoja na Wizara ya
Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ili kuhakikisha wakulima wanapata taarifa bora.
No comments:
Post a Comment