NMB
YAENDELEA KUZINDUA BUSINESS CLUB “SASA
NI ZAMU YA KARATU”
Benki ya NMB imeendelea kuwa kinara katika kubuni na
kuboresha huduma mbali mbali za kibenki, ili kuwawezesha wateja wake kupata
unafuu na urahisi wa upatikanaji wa huduma za kibenki nchini Tanzania.
Katika kulizingatia hili, NMB imezidi kuzindua klabu
maalum za wafanyabiashara maarufu kama NMB Business Club. Hadi sasa zaidi ya NMB
Business Club 29 zimekwisha zinduliwa nchi nzima.
Kupitia NMB Business Club wajasiriamali wanaowezeshwa
na benki ya NMB wamekua wakipata nafasi ya kujifunza jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara zao na pia
kuendelea kua vinara wa biashara.
Mhandisi Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Tulinumpoki Mwakalukwa akitoa shukrani
zake kwa NMB mara baada ya kuzindua
rasmi NMB Business Club wilaya ya Karatu. Kushoto ni Meneja wa NMB
tawi la Karatu , Evarist Mtaro na Mkuu wa Kitengo cha wajasiriamali
wadogo wadogo na wakati wa NMB, Filbert
Mponzi.
Sehemu ya wanachama wa NMB Business
Club wilaya ya Karatu wakifurahia uzinduzi wa NMB Business Club.
Mkuu wa Kitengo cha wajasiriamali
wadogo wadogo na wakati wa NMB, Filbert Mponzi akimkabidhi mwenyekiti
wa NMB Business Club, Paulith Jack mara baada ya kuibuka kidedea kwenye
mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa NMB Business Club Karatu .
No comments:
Post a Comment