PARIS, Ufaransa
NYOTA wa tenisi duniani, Rafael Nadal jioni hii amefanikiwa
kutwaa ubingwa wa Michuano ya Wazi ya Ufaransa ‘French Open’ akivunja rekodi ya
kubeba kwa mara ya nane.
Nadal alifanikiwa kubeba French Open 2013 kwa kumduwaza
Mhispania mwenzake David Ferrer kwa seti tatu mfulizo za 6-3 6-2 6-3.
Nyota huyo mwebnye umri wa miaka 27, anakuwa mtu wa kwanza
kutwaa ubingwa Grand Slam nane.
Nadal alilazimika kupigana kiume kumshinda Ferrer,
aliyeonesha umahiri wa kuokoa katika seti ya kwanza ya pambano hilo ambalo ni
fainali kubwa ya kwanza kwa Ferrer.
Mechi hiyo ililazimika kusimama kwa kupisha, kupisha askari
kumuondoa dimbani shabiki aliyeingilia mchezo dimbani na kufyatua fataki za
moto.
BBC Sport
Nadal akishangilia ushindi katika seti ya kwanza dhidi ya David Ferrer.
Nadal akijuta kushindwa kuzuia.
Kushoto; Askari akimuo shabiki aliyevamia dimba la Roland Garros. Kulia: Askari akimlinda Nadal asishambuliwe.
Shabiki akivamia dimbani akiwa na fataki la moto na kusababisha mechi kusimama kwa muda hadi alipookolewa.
Nadal akiokoa mkwaju wa Ferrer katika mechi yao ya fainali kwenye dimba la Roland Garros.
Rafael Nadal akitumia mkono wake wa kushoto kurudisha mpira kwa Ferrer.
Ferrer akiwajibika katika mtanange huokuwania Grand Slam.
David Ferrer akirudisha mpira kwa mpinzani wake Rafael Nadal (ambaye hayuko pichani).
No comments:
Post a Comment