Kwa mara nyingine limeandaliwa pambano la ngumi la ki aina
yake ni kati ya mabondia wakimya na wapole usoni na wasiopenda kabisa kuongeaYohana
Robert aliekuwa bondia wa taifa na
mkongwe katika masumbwi atakapopigana na Yohana Mathayo katika ukumbi wa
friends corner manzese siku ya jumapili
tarehe 30 mwezi huu.
Pambano hilo linakuwa la kiana yake kwa sababu ya sifa za
hao mabondia kuwa ni wacha mungu wazuri
kiasi cha yohana Robert kuitwa na wapenzi wa masumbwi “mtakatifu ngumi jiwe” ni mtu mwenye ngumi mojamoja
ambazo ni nzito sana na hatari kwa
mpinzani nae bondia Yohana Mathayo
wapenzi humwita “Tembo mtoto”
kutokana na umbo lake kubwa, pia humwita “Yohana mbatizaji” kwani mara
nyingi huwaachisha ngumi wapinzani wake
kwa kipigo au kubadilisha majina yao, mathayo ana ngumi kali za kuvizia,
hutulia muda mrefu na akiachia ngumi moja ikikupata vizuri mchezo umekwisha ni
mtaalamu wa kuvizia.
Pambano hili limeandaliwa na mwalimu Hatibu ambae ni mdau wa
karibu wa ngumi na tunaliita pambano la aina yake kwa mabondia wote kufanana
majina na matendo na huwa na tabia ya kubeba na kusoma biblia kabla na baada ya
pambano ni wapole watulivu lakini ni watu hatari sana ulingoni na lolote laweza
tokea wanapocheza.
Pambano hilo ambalo
litasimamiwa na PST chini ya Anthony
ruta na mapambano ya utangulizi kuratibiwa na Ibrahim kamwe bigright.
Mwalimu Hatibu
anaripoti ya kuwa maandalizi yanakwenda
vizuri vibali vyote tayari na mabondia
watakaowasindikiza kina Yohana na mikataba yao imekwisha kamilika ni Fabian
lyimo ambae pambano la mwisho alifanya vizuri Indonesia atazipiga na
musa sunga nae Bakari ustadh atazipiga na frank zagarino, wakati huohuo Tasha
mjuaji na Rama johncena watatoana jasho.
Pia Yule bingwa wa
PST uzito mdogo (minimum weight) goldsilver anaumana vikali na herman Richard.
Nae Ibrahim kamwe anathibitisha hilo na linaweza kuwa pambano kali sana la
vunja jungu ambalo halijawahi kutokea kutokana na sifa za mabondia hao.
IBRAHIM KAMWE
+255 -713 / 767 / 784 - 501991
kamwe@hotmail.com
No comments:
Post a Comment