KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme (Tanesco), Felchesmi Mramba amesema kuwa, asilimia 90 ya ukatikaji wa umeme nchini unasababishwa na miti kugusa nyaya.
Mramba alisema hayo leo baada ya kukabidhiwa kituo cha kupozea na kusambaza umeme na mwakilishi wa Jica Yasunori Onishi, baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa na JICA. Kituo hicho kipo Ilala Mchikichini, Jijini Dar es Salaam.
Alisema kutokana na hali hiyo, wataanza mkakati maalum wa kukata miti hiyo.
“Tunaanza na Mkoa wa Dar es Salaam, tumeshawasiliana na wakurugenzi wa manispaa za mkoa huu,” alisema na kuongeza kuwa, kwenye line kubwa miti inapokuwa na unyevu kidogo ikigusa nyaya inaleta shida na kusababisha kukatika kwa umeme.
Alisema kuwa, katika mkakati huo watachukua tahadhari ili wasikate miti ambayo haiathiri umeme.
Kwa mujibu wa Mramba, uhusiano mzuri walionao na serikali ya Japan umeweza kujenga chuo ambacho kinaandaa wahandisi na fundi mchundo ili waweze kufanya kazi kwa viwango.
Mkurugenzi wa
Tanesco, Felchesmi Mramba (wa tatu kushoto) na mwakilishi wa shirika la kimataifa la JICA,
Yasunori Onishi wakikagua mitambo ya kusambaza umeme katika kituo cha Ilala
Mchikichini jijini Dar es Salaam, baada ya JICA kukabidhi kituo cha kusambaza umeme cha Ilala Mchikichini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco.
No comments:
Post a Comment