Naibu
Waziri wa Fedha, Janet Mbene akiweka sahihi katika kitabu cha wageni alipotembelea banda la NSSF. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Katavi, Anna Lupembe.
Naibu Waziri wa Fedha akipata maelezo ya shughuli za NSSF.
Mmoja wa wanachama wa NSSF akijaza fomu ya kujiunga na mpango wa hiari wa kuchangia mafao.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene akiangalia mchoro wa jengo la Hospitali ya Apollo itakayokuwa ikitoa matibabu ya magonjwa ya moyo pamoja na Chuo cha Utabibu na Dawa eneo la Kigamboni jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja Kiongozi Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akimpa maelezo kuhusiana na hospitali hiyo.
Wengi walivutiwa na huduma za NSSF.
Huduma za matibabu.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene akizungumza na waandishi wa habari.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Katavi, Anna Lupembe.
Baadhi ya watoto waliotembelea banda la NSSF wakipata zawadi ya madaftari kutoka kwa Ofisa wa NSSF, Silvia Mashuda.
Wateja wa Sh,irika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakisubiri kupata huduma katika banda la shirika hilo katika viwanja vya Sabasaba.
Na Mwandishi Wetu
NAIBU Waziri wa Fedha, Janet Mbene amesema lengo la kuzitembelea taasisi za kifedha na nyingine zilizoko chini
ya Wizara hiyo ni kutaka kujua mafanikio na changamoto za taasisi hizo.
Mbene amesema hayo wakati
alipotembelea banda la maonesho la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Alisema baada ya kutembelea
na kuangalia banda hilo, alibaini kuwa changamoto kubwa ni fedha ambazo
zinahitajika kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma za mfuko huo, kwa kutumia
teknolojia ya kisasa.
Mbene alisema baada ya
kubaini hayo serikali inao wajibu wa kutafuta kila njia lengo likiwa ni
kuzipatia ufumbuzi wake.
Unajua hivi sasa kila kazi
zote zinafanywa kwa kutumia mfumo wa teknolojia ambao kwa kawaida ni mahususi
katika kurahisisha kazi na kuifanya iwe bora zaidi”alisema Mbene.
Mbene alisema ukiachilia
mbali uhitaji wa teknolojia bado pia wataalam ambao wangetumika kusimamia
mifumo hiyo hawatoshi, serikali kwa kuliona hilo itahikikisha kuona
wanapatikana.
Akizungumzia kuhusu mafanikio
ya Mfuko wa NSSF, Eunice Chiume alisema mfuko huo hivi sasa umepiga hatua
katika kuwafikishia huduma mbalimbali wateja wake kila kona ya nchi na nje.
Aidha, Mfuko huo katika
kuboresha maisha ya wafanyakazi wake inatoa mikopo, hata hivyo masharti ya
kupata mkopo huo ni lazima muombaji awe mwanachama wa SACCOS.
No comments:
Post a Comment