Mshambuliaji Lionel Messi akitafakari mchezo ulivyokuwa ukienda wakati Barcelona ilipokuwa ikiumana na Atletico de Madrid na kutoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Vicente Calderon kuwania ubingwa wa Spanish Super Cup.
Hapa Messi akipiga shuti kwa mguu wa kushoto, dakika chache kabla ya kuumia na kutolewa wakati wa mapumziko na nafasi yake kujazwa na Cesc Fabregas. Wakati bao la Barca lilifungwa na Neymar, bao la Madrid lilifungwa na nyota wa zamani wa Barcelona, David Silva.
Messi akisikitika baada ya kukosa moja ya nafasi kabla hajaumia na kutolewa wakati wa mapumziko.
Neymar akiisawazishia Barcelona kwa kichwa wakati wa mechi mechi. Hilo ni bao la kwanza kwa Neymar tangu aliposajiliwa Barcelona kwa dau la pauni milioni 48 akitokea Santos ya Brazil.
Neymar akishangilia bao hilo ambalo Mkurugenzi wa Michezo wa Barca alilishangaa na kusema: 'Kama tungeambiwa bao la kwanza la Neymar akiwa Barca litakuwa la kichwa, tusingekubaliana na hilo, kwa sababu hakuna aliyetarajia kijana huyu kufunga bao la aina hii.'
David Villa akishangilia bao la uongozi la wenyeji Atletico Madrid, alipokutana na nyota wenzake wa zamani wa Barcelona aliyoihama kiangazi hiki na kutua Madrid.
David Villa akishangilia bao hilo la dakika ya 12, ingawa halikuweza kuwapa ushindi wa nyumbani. Madrid na Barcelona zinarudiana Jumatano ijayo Nou Camp kusaka mshindi wa Spanish Super Cup.
Villa akiendelea na ushangiliaji wake baada ya bao hilo.
mshambuliaji wa Atletico Madrid, Diego Costa akichuana na Jordi Alba wa Barcelona katika mtanange huo wa kukata na shoka.
Mlinda mlango wa zamani wa Chelsea, Thibaut Courtois anayedakia Madrid kwa sasa, na mabeki wake Filipe na Diego Godin wakifanya kazi ya ziada kuokoa mpira uliopigwa na Alexis Sanchez usitinge nyavuni kwao. Walifanikiwa!!!
Sanchez wa Barca akimtoka kiungo mahiri wa Atletico Madrid, Mario Suarez.
Miranda wa Madrid akijaribu kupiga shuti huku akizongwa na Pedro wa Barcelona.
No comments:
Post a Comment