DAR ES SALAAM, Tanzania
Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa kimepinga uamuzi wa kuwafukuza madiwani nane wa Chama hicho
na kuwaondoa nyadhifa zao uliofanywa na Chama hicho katika Mkoa wa Kagera
waliokuwa wamesaini hati ya tuhuma za ufisadi ili kumng’oa Meya wa Manispaa ya
Bukoba Anatory Amani, kutimuliwa madiwani hao kulikuwa kunapelekea uchaguzi
mdogo katika kata nane za Jimbo la Bukoba Mjini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za
Makao makuu ya Chama hicho, Katibu wa Halmashauri kuu ya taifa, Itikadi na
Uenezi Nape Nauye alisema
“kwa mujibu wa utaratibu wa kutoa adhabu kwa viongozi wa CCM walio
kwenye vyombo vya dola hasa Wabunge na madiwani, uamuzi wa Halmashauri kuu ya
mkoa sio wa mwisho".
Kwani unapaswa kupata baraka za Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ndipo utekelezwe
Kutokana ana msimamo huo, Nape alisema kuwa madiwani hao
nane waliosimamishwa wanapaswa kuendelea na kazi zao kama kawaida wakisubiri
kikao cha kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachoketi Dodoma 23 Agosti
mwaka huu.
Licha ya maamuzi hayo kutolewa juzi usiku, Katibu huyu
aliwahakikishia waandishi wa habari kuwa alikuwa tayari amepokea barua za
madiwani hao waliokata rufaa kupinga uamuzi wa kufukuzwa nyadhifa zao,
Katika kujibu maswali ya waandishi, Nape alilaumu vyombo vya
habari kuwa vilimnukuu vibaya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika
akauli aliyoitoa akiwa Bukoba hivi karibuni ya kuwasihi Mbunge wa jimbo hilo
Hamisi Kagasheki na Meya huyo wapatane.
No comments:
Post a Comment