HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 30, 2013

KING CRAZY GK AIBUKA UPYA


Na Elizabeth John

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la East Coast Team, Gwamaka Kailunga ‘King Crazy GK’ ameibuka na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Baraka au Laana’ ambao amemshirikisha chipukizi wa muziki huo, Yuzo.

Crazy GK alishawahi kutamba na vibao vyake vingi vikiwemo vya ‘Leo’,  ‘Nitakufanyaje’, ‘Sister’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, GK alisema, amejipanga kurudi upya katika fani hiyo na anawaomba wapenzi wa muziki huo wakae mkao wa kula kwaajili ya kukipokea kibao hicho ambacho kitaanza kusikika wiki ijayo katika vituo mbalimbali vya redio.

“Naomba wapenzi wangu wakae mkao wa kula kwaajili ya kuipokea kazi hii ambayo naamini itafanya vizuri kutokan ana ubora wa mashairi ya wimbo huu na maudhui yake,” alisema.


Msanii huyo ambaye alipotea kwenye ‘game’ kwa kipindi cha miaka kadhaa, alisema amerudi kivingine katika fani hii na amewataka wapenzi wa muziki huo kukaa mkao wa kula kukipokea kibao hicho ambacho atakisambaza pamoja na video yake.

No comments:

Post a Comment

Pages