Na Bryceson Mathias
YESU aliwaambia Wanafunzi na Wafuasi wa njia hii ni hiki. “Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang'anyi. Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo”.Yohana 10:1-2.
Kwa maana ya Mtume huyu ‘Yesu’, kama kuna mtu anatokea tena anaitwa Mchungaji, halafu anaingia zizini kwa kupitia dirishani, huyo lazima tumwite Mwivi, na mbali ya Uizi tumwite mchungaji wa Mbuzi, na si Kondoo.
Sifa za Mchungaji wa Kondoo ambaye huwa muwazi kwa kupita mlangoni badala ya Dirishani, zimeelezwa na Yesu kuwa, Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje.
Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. Yesu akifafanua Sifa ba Ueledi wa Kondoo anayechungwa na Mchungaji alisema,
“Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni”. Anasema, Mithali hiyo Yesu aliwaambia, lakini wao hawakuelewa na mambo hayo aliyowaambia.
Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo. Akasisitiza,
“Wote walionitangulia ni wevi na wanyang'anyi; lakini kondoo hawakuwasikia. Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho”. Lakini akaonya, Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele”.
Yesu akaendelea kujitambulisha kwamba, “Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya.
“Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake. Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi; kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo.
Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.
“Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena. Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu”. Yesu alipimzisha Kaulisha yake katika Yohana 10:18.
Hivi karibuni tulihabarishwa na Mwandishi, Julius Kunyara, kwamba Kamati ya Utendaji ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Ukonga iliwafukuza uanachama wanachama wake wanane huku wawili wakipewa onyo kali kwa tuhuma za kukihujumu, kutokana na kwamba si wa Zizi la Chadema, na hawamjui Mchungaji wao kwa jina, hivyo huweza kudanganywa, wakala hata mazao ya watu.
Baada ya kusoma taarifa hizo na kubaini kondoo hao waliponzwa na Mchungaji aliyetambulishwa kwa jina la, Zabron Shilinde, na Mswagaji, Habibu Rajabu, niliwasikitikia Kondoo hao waliobadilishiwa majina wakawa Mbuzi, walioponzwa kwa kupitishwa dirishani wakakwea penginepo.
Mbali ya Mchungaji na Mswagaji huyo kukifanyia Mchezo mchafu Chadema,hata kama angekifanyia Chama tawala CCM), mtumishi huyo amezidharirisha Taasisi ya Dini kwa ujumla wake, badala ya kuwapeleka watu kwa Mungu amewapeleka kwa Shetani, maana lazima aliwarubuni kwa rushwa; na Biblia inakataza.
Kama Mchungaji anaweza kumshawishi Muumini au Kondoo afanye hayo, si anaweza kumpeleka kwa hata kwa Mganga wa Kienyeji akaague au Kuroga? Anashindwaje kuwashawishi watu wakaua au kuwamwagia watu tindikali? Mtu wa namna hiyo anashindwaje kuwa mchochezi?
Ndiposa nimeuliza, Mchungaji aliyevuliwa uongozi na chadema ni wa Kondoo au Mbuzi? Kimsingi binafsi nilimtegemea awe kielelezo.
Isaya 56:1-3 Biblia inasema, “Bwana asema hivi, Shikeni hukumu, mkatende haki; kwa maana wokovu wangu u karibu kuja, na haki yangu kufunuliwa. Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye sana; azishikaye sabato asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wo wote”. Sielewi warubuni hao kama wanayafahamu haya!
“Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia;huota ndoto, hulala, hupenda usingizi. Naam, mbwa hao wana choyo sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote. Husema, Njoni, nitaleta divai, Na tunywe sana kileo; Na kesho itakuwa kama leo, Sikukuu kupita kiasi. Isaya 58:10-12.
0715-933308
No comments:
Post a Comment