Na Denis Mlowe, Iringa
WATU wawili wamefariki dunia kwa kuzama maji akiwemo mtoto Gift Kadafu (2.5) mkazi wa kijiji cha Kitanzini Ndiwili, Wilaya ya Iringa,aliyefariki dunia baada ya kuzama kwenye Mto Ruaha.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 22 saa 10:00 jioni mtoto akiwa na mama yake kando kando ya mto Ruaha.
Mungi alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kuweza kubaini nini chanzo kutokana na kuonekana kuna uzembe kwa mtoto huyo kuzama hadi kufariki akiwa na wazazi jirani.
Mungi alisema chanzo cha kifo hicho ni uzembe wa wazazi wake wa Matalawe alikamatwa kutokana na ushirikiano mzuri baina ya jeshi la polisi na askari wa wanyama pori wa hifadhi ya taifa ya Ruaha..
Katika tukio jingine lililotokea maeneo ya Luhanga kata ya Nyabula wilaya ya Iringa Fausta Mhulo (54 alifariki dunia baada ya kutumbukia kwenye kisima cha maji kilichopo karibu na nyumba yake.
Mungi alisema kifo hicho kilitokea majira ya saa 3 usiku chanzo cha kifo hicho ni ugonjwa wa akili aliokuwa nao marehemu .
No comments:
Post a Comment