HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 23, 2013

Ubovu wa Katiba iliyopo!

Na Bryceson Mathias
 
Chuma hakiunganishwi na udongo’, Kikiunganishwa huachia.
 
WANANCHI wengi na Wanasiasa, wamekuwa wakishutumu sera mbovu zilizopo za ‘kuwabeba’ wageni (wawekezaji), kutokana na Serikali kuwamilikisha ardhi na kuwaacha wazawa wanyonge wakiteseka bila kuwa na sauti kuhusu ardhi yao inayochukuliwa.
 
Nia ya wananchi wanataka,“Mwekezaji anapokuja kutoka nje anataka kuwekeza katika ardhi, aje moja kwa moja kwa mwananchi mwenye ardhi hiyo na aingie naye mkataba mzawa mwenyewe.
 
Hiyo ndiyo imekuwa moja ya mipango ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikiwa na lengo la kumpa mwananchi uwezo wa kumiliki rasilimali ya nchi yake mwenyewe.
 
Kimsingi wazo zuri la Chadema linaloonekana ni ukombozi kwa wananchi, haliwezi kufannikiwa kama hakutakuwa na hatua za makusudi za zitakazofanywa kufuta kipengele cha katiba inayoitwa kiraka kibovu cha sasa kinachosema, Ardhi ni mali ya Serikali.
 
Kwa mtazamo wangu, ili kuwasaidia wananchi  kuondokana na umaskini wa kutpwa, Serikali iliyopo madaraka isitumie Fursa ya kujadili Rasimu ya Katiba kuchomeka na kulinda mambo yake badala yake ilenge mambo ya msingi kama vile afya, elimu, uchumi  na Maadili.
 
Sera ya kukumbatia maovu, kama ya Kuku kukumbatia vifaranga, kwa sehemu kubwa imeathiri sekta nyingi za utendaji ndani ya serikali na Jamii, ambapo sasa tunashuhudia msururu wa watoto na ndugu wa vigogo nchini, ndio wanaohusika na madawa ya kulevya.
 
Ndiyo maana waswahili husema, huwezi kuunganisha chuma na udongo, na ukiunganisha, kwa vyvyote lazima ukiweka maji (ukweli) kitaachia tu.
 
Ni ukweli ulio wazi kwamba, Kimsingi watawala wetu hawawezi kuhubiri Amani, Rushwa, Ufisadi, Udhibiti wa Madawa ya Kulevya, Maisha Bora kwa kila Mtanzania, Kilimo Uti wa Mgongo, Matokeo Halisi Sasa (Big result Now) majukwani, bila kumaanisha.
 
Huo ni wimbo wa Jogoo wa kuwataarifu watu wenye nyumba kuwa waamke kumekucha, wakati Jogoo mwenyewe hawezi kufungua Mlango.
 
Wengi wa viongozi wa Serikali, Vyama vya Siasa na baadhi ya Viongozi wa Dini, wamebaki kuwa kama Jogoo, wanapiga kelele majukwani na kwenye Makanisa na Misiti, lakini hawawapeleki wananchi kwenye kusudi la kupata Haki na rasilimali zao, isipokuwa kuwatesa.
 
Viongozi wengi wa Dini, wamekuwa wakidanganywa na Harambee kwenye dini zao, wananchi wakidanganywa na Tisheti, Kanga na Ubwabwa na Nyama ambao ni mulo wa siku moja, na kuchagua viongozi wabovu ambao watawaumiza kwa miaka mitano.
 
Kutokana na Katiba Mbovu tuliyonayo wakati tumeridhia kuwa na Demokrasia  ya vyama vingi, yapo mambo mengi ambayo watawala walitakiwa wawe wamekwisha yaondoa katika Katiba, ikiwemo tume ya uchaguzi isiyo huru, uchelewashaji wa matokeo kwa analojia nk.
 
Mahali tulipo sasa, ni pabaya sana kwa sababu, kwa njaa ya kipato, chakula, malazi na mavazi; itafika wakati mtu akiwa na unga njiani, atanyang’anywa alichonacho, kupigwa na hatimae kuuawa bila Serikali au vyombo vya Usalama na Sheria kuchukua hatua.
 
Hali hiyo inatokana na mfumo wetu Mbovu wa ulinzi na usalama tangu serikali za mitaa hadi Serikali Kuu, ambapo kwa siku za hivi karibuni kumeonekana kuna mapungufu ya uwajibikaji, ambapo wananchi wanatendewa uovu mchana kweupe!
 
Aidha ni wakati muafaka sasa, Serikali na Sekta mbalimbali hasa kwa kila Mtanzania na Kila mwenye mapenzi mema na Amani, Maendeleo, na Mustakabali mzima wa Taifa na Wananchi wa Tanzania. nyeregete@yahoo.co.uk 0715933308

No comments:

Post a Comment

Pages