MSANII wa muziki wa kizazi kipya
kutoka Nyumba ya Kukuza Vipaji Tanzania (THT), Ally Nipishe, anatarajiwa
kusambaza ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Kwea pipa binadamu’, hivi
karibuni.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ally Nipishe alisema anashukuru wimbo wake wa ‘My’ umekubalika na amekuwa
akipata shoo mbalimbali ndani ya Dar es Salaam, katika kazi hiyo kamshirikisha
mkali wa muziki wa mduara nchini, Ally Ramadhan ‘AT’.
“Nashukuru Mungu kwamba toka
nimetoa wimbo wangu wa ‘My’ unaendelea kufanya vizuri, umekubalika kwa haraka
kwa sababu nimetoa ujumbe ambao ni wa kuelimisha jamii, pia napata shoo,”
alisema.
Ally Nipishe alisema, baada ya
kuusambaza ‘Nikupulike’, ambao umeanza kufanya vizuri katika redio mbalimbali,
anajipanga kusambaza video yake kabla ya kuisambaza ngoma hiyo mpya.
Msanii huyu kipaji chake kilianza kuvuma pale
aliposhirikishwa na msanii wa kike, Mwasiti, katika kazi yao inayokwenda kwa
jina la ‘Ni Wewe’, ambako alionekana kufanya vizuri na mashabiki kumtaka atoke
na wimbo wake.
No comments:
Post a Comment