HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 16, 2013

Clara ndiye Redd’s Miss Sportwoman

Clara Bayo wa kwanza kulia.

Na Mwandishi Wetu

MREMBO Clara Bayo anayetoka Kanda ya Mashariki juzi jioni alifanikiwa kutwaa taji la Redd’s Miss Sportwoman na hivyo kupata fursa ya kuingia 15 Bora ya shindano la Redd’s Miss Tanzania.
 
Kutokana na ushindi huo, Clara anaungana na warembo wengine watatu kuingia katika hatua hiyo ambao ni Happiness Watimanywa (Redd’s Miss Photogenic), Narietha Boniface (Redd’s Miss Top Model) na Prisca Clement (Redd’s Miss Talent).
 
Clara alifanikiwa kushinda taji hilo kutokana na kuonyesha uwezo mkubwa katika michezo mbalimbali katika mashindano maalumu yaliyofanyika katika fukwe ya Kunduchi, Dar es Salaam.
 
Akizungumza mara baada ya kutangazwa ndiye mshindi, Clara alisema alikuwa na uhakika mkubwa wa kutwaa taji hilo na anaamini kile alichodhamiria ndicho kilichotokea.
 
“Lengo langu ni kutwaa Redd’s Miss Tanzania kwa mwaka huu, najiamini katika hilo na naamini nitafanikiwa,” alisema.
 
Meneja wa Redd’s Original, Victoria Kimaro alitoa pongezi zake kwa mshindi huyo na kusema, anaamini warembo wengine nao watahakikisha wanafanya kweli ili kutwaa taji la Redd’s Miss Tanzania.
 
“Mwaka huu shindano hili lina ushindani mkubwa kwani warembo wote wana sifa zinazostahili,” alisema.
 
Shindano la Redd’s Miss Tanzania linatarajiwa kufanyika Jumamosi Sepetemba 21, katika ukumbi wa Mlimani City uliopo Mwenge, Dar es Salaam.
 
Kinyang’anyiro cha Redd’s Miss Tanzania kwa sasa kinadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

No comments:

Post a Comment

Pages