HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 13, 2013

KINANA AHITIMISHA ZIARA YAKE KISHAPU KWA MAFANIKIO MAKUBWA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi waliofika kumpokea kwenye wilaya ya Kishapu katika eneo la Maganzo ambapo Katibu Mkuu alikuwa na ziara katika wilaya ya Kishapu.
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi moja ya madarasa katika shule ya Sekondari Mwigumbi.
Moja ya Nyumba mpya iliyojengwa kwa ajili ya makazi ya Walimu wa Shule ya Sekondari Mwigumbi, wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga ambayo ilizinduliwa leo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitumia usafiri wa baiskeli kufika kijiji cha  Mwigumbi ambapo kulikuwa na shughuli za kuzindua mradi wa maji.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kuzindua mradi wa maji wa kata ya Mondo,kijiji cha Mwigumbi wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga.
 Mbunge wa Kishapu Suleiman Masoud Mchambi akishiriki kucheza ngoma ya kiasili wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji uliofanyiaka kata ya Mondo kijiji cha Mwigumbi.
 Tanki la maji litakalowasaidia wakazi zaidi ya 4000 katika kijiji cha Mwigumbi ,pichani wakazi wa kijiji hicho wakiwa wamekusanyika kushuhudia uzinduzi rasmi wa tanki hilo.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mwigumbi mara tu baada ya kuzindua mradi wa maji utakaosaidia zaidi ya watu 4000.
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Ndugu Azah Hilal Hamad akiwahutubia wakazi wa kata ya Mondo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Mwigumbi.
 Mbunge wa Kishapu Ndugu Suleiman Masoud Mchambiakihutubia wakazi wa kata ya Mondo na kuelezea namna gani jimbo lake limekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama cha Mapinduzi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiingia kwenye viwanja vya Mabela kwa staili ya aina yake tayari kuhutubia wakazi wa Wilaya ya Kishapu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza  Balozi wa China hapa nchini ndugu Lu Youqinq wakati wa mkutano wahadhara uliofanyika katika viwanja vya Mabela, kushoto kwake ni Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.

No comments:

Post a Comment

Pages