HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 10, 2013

Ndugai alipotaja mapungufu ya wapiga kura wake na ya Watanzania

Na Bryceson Mathias
NAIBU Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai, katika Mkutano wa 12 wa kikao cha 2 cha Bunge Dodoma Jumatano, Agost 28, 2013, alishindwa kuvumilia na kuficha hisia zake akataja mapungufu waliyonayo wapiga kura wake na watanzania dhidi yake.
Dungai alitoa kauli hiyo kabla ya kumpongeza Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Njombe, Anne Semamba Makinda, ambaye hivi karibuni alichaguliwa kuwa Rais wa Mabunge ya Afrika kwa Jumuia ya Madola.
Bila kuuma maneno Ndugai alisema,”Watanzania wamekuwa na mapungufu ya kutoenzi kazi nzuri zilizofanywa na viongozi na kuwapongeza walipofanya vizuri, badala yake wamekuwa wakitanguliza Lawama za kuwalaumu, jambo linalokatisha tamaa na kipunguza Moyo wa kujituma”.
Ndugai alitolea mfano wa jimboni kwake ambako alisema, hakuna Mradi wowote kwa mfano Ujenzi wa Choo, Zahanati, Shule na Maendeleo mbalimbali yanyofanywa bila Mchango wake kuhusika, lakini hata siku moja hakuna Mradi wowote ambao aliofanywa mgeni rasmi na kuufungua.
Nimekuwa nikitoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya Jimbo langu, hakuna kinachofanywa ambacho sihusiki kuchangia, lakini ikifika wakati wa ufunguzi, wanafungua wengine hivyo hadi nitakapomaliza kipindi change sina kumbukumbu yoyote”.alisema Ndugai.
Alichosema Ndugai ni ukweli usiopingika, kwani hivi karibuni nilifanya Ziara kati shule moja ya Msingi ya NDC-NARCO Kongwa, ambayo baadhi ya Wabunge katika Bunge lililopita walijitolea kuichangia ili kumalizia Jengo la Kulala, lakini Viongozi wa Elimu (W) walisita kumwalika na badala yake walitaka kumualika Mbunge mwingine.
Mmoja wa viongozi hao wa Wilaya ya Kongwa alifikia mahali pa kumtishia Mwalimu mmoja Jina linahifadhiwa, asijihusishe na Wanasiasa katika kufanikisha Ujenzi huo na badala ya anamtaka afundishe, la sivyo akifanya Mchezo atamhamisha.
Hoja yangu ni kwamba, ni kwa nini Kiongozi mkubwa namna hiyo tena Naibu Spika Bunge (Ndugai) hata Jengo au Barabara jimboni kwake lisiitwe kwa Jina lake? Swala hili ndilo linamsibu Ndugai hata akatafuta mahali pa kufikisha Ujumbe kwa wananchi wake na watanzania.
Pamoja na kwamba kuna usemi usemao ajikwazaye atashushwa na ajishushaye atakwezwa, tujiu;ize; Je. Kwa nini wananchi wa Jimbo la Kongwa, Viongozi wa Mkoa wa Dodoma na Tanzania hawammpi fursa anayojipigia debe Mbunge huyo hadi aipigie chapuo akipongezwa Makinda?
Wananchi na viongozi jimboni humo waliohojiwa kwa nyakati tofauti na kuombwa wasitajwe majina yao walidai,
 “Ni kweli sisi kama viongozi wa Elimu wilayani humu, tumekuwa tukimuita Mbunge wetu mara kadhaa kwa ajili ya kuchangia shughuli mbalimbali za Elimu, lakini amekuwa si mtoaji na mshiriki wa karibu wa shughuli husika”.alisema mdau mmoja wa elimu wasioiva wilayani humo.
Mkulima mmoja wa Mahindi na Alizetiwengi miongoni mwa wenzake wa Kijiji cha Pandambili wilayani Mlali alimtuhu kama alivyowahi kumshitaki Meya wa Musoma Alex Kasurura (Chadema) katika moja ya Mikutano jimboni humo kwamba, Ndugai ameshindwa kuwatafutia Masoko ya mazao hayo wananchi wake ingawa anajisifu kwa safari za kwenda nje kila mara.
Aidha katika Malalamiko ya Ndugai dhidi ya Wapiga kura wake na Watanzania kuwa hawampi nafasi au Fursa za kumuenzi hata kwa kumpa kumbukumbu za Majina ya Miradi ya Barabara au Majengo ni kutokana na kutokuwa na ushirikiano wa karibu na watu wake. Ajihoji.

No comments:

Post a Comment

Pages