Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba, wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole, Mjini Unguja, baada ya kumwagiwatindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi jana jioni, Padri alimwagiwa Tindikali alipokuwa akitokakupata huduma ya Mtandao. (Picha na Ramadhan Othman, Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein,akimsikiliza Padri Joseph Monesmo agamba,waKanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,akitoa maelezo jinsi alivyopata mkasa wa kutiwa Tindikali na watu wasiojulikanwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein,akiwafariji jamaa na wafuasi wa Padri Joseph Monesmo Magamba.
Mmoja wa Ngugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,waKanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,akimueleza Rais waZanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, hisia zake kwa Uchungu kutokana na kitendo hicho cha kumwagiwa Tindikali na watu wasiojulikanwa kwamba zilichukuliwe hatua za kisheria na kukomeshwa Vitendo kama hivyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akifafanua jambo wakati alipokuwa
akiwafariji jamaa na wafuasi wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, waliofika kumuangalia Padri huyo aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kumwagiwa
Tindikali.
No comments:
Post a Comment