LONDON, England
Mabingwa watetezi, Manchester United watakuwa nyumbani
Old Trafford, kuwaalika Crystal Palace, katika mechi ya mapema, itakayofuatiwa
na nyingine sita tofauti kwenye viwanja vya Villa Park, White Hart Lane, KC,
Britania, Light na Craven Coattage
BAADA ya mapumziko kupisha mechi za kimataifa kuwania kufuzu
Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil, timu 16 kati ya 20 za soka za Ligi Kuu ya
hapa leo zinajitupa kwenye viwanja nane tofauti kuwania pointi muhimu.
Mabingwa watetezi, Manchester United watakuwa nyumbani Old
Trafford, kuwaalika Crystal Palace, katika mechi ya mapema leo, itakayofuatiwa
na mechi sita tofauti kwenye viwanja vya Villa Park, White Hart Lane, KC,
Britania, Light na Craven Coattage.
Wenyeji wa dimba la Villa Park, Aston Vila watakuwa hapo
kuwaalika Newcastle United, huku Tottenham ikiumana na Norwich City huko White
Hart Lane jijini hapa, na Hull City ikitunishiana misuli na Cardiff City huko
kwenye Uwanja wa KC.
Manchester City na Arsenal zina nafasi ya kupaa kileleni mwa
msimamo wa ligi hiyo, kama zitaweza kuibuka na ushindi mnono kwenye viwanja vya
ugenini, ambapo Man City itakuwa Britania kuwavaa wenyeji Stoke City, huku
Arsenal ikiwa Light dhidi ya Sunderland.
Wenyeji wa Uwanja wa Craven Coattage, Fulham watakuwa
nyumbani kuwaalika West Brom Albion, ambapo mechi ya mwisho kabisa jioni ya leo
itakuwa baina ya Everton, watakaowakaribisha Chelsea, kwenye dimba la Goodison
Park.
Vinara wa ligi hiyo kabla ya mechi za leo, Liverpool
watakuwa mapumziko kwa muda zaidi hadi Jumatatu, watakaposafiri kuwafuata
Swansea City kwenye dimba la Liberty, wakati kesho Jumapili, Southampton
watawaalika West Ham kwenye Uwanja wa St Mary’s.
Ratiba mechi za leo Ligi Kuu ya England
Man Utd v Crystal Palace - saa 8:45
Aston Villa v Newcastle - saa 11:00
Tottenham v Norwich - saa 11:00
Hull v Cardiff - saa11:00
Stoke v Man City - saa 11:00
Sunderland v Arsenal - saa 11:00
Fulham v West Brom - saa 11:00
Everton v Chelsea - saa 1:30
Supersport.com
No comments:
Post a Comment