HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 07, 2013

Rais Kikwete ziarani Misungwi

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni wakati alipowasili katika Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kuanza ziara ya kikazi leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mwanzilishi na Mkurugenzi wa Shirika la Africa School Home Bibi.Aimee Bessire wakufunua kitambaa katika jiwe lamsingi kuashiria kuzindua rasmi Shule ya msingi Ntulya.Shule hiyo imejengwa kwa ufadhili wa Shirika la Africa School Home lenye makao yake nchini Marekani. (Picha na Freddy Maro)
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa kumbukumbu muda mfupi baada ya kuzindua rasmi Shule ya msingi Ntulya,iliyopo kata ya Mondo, Wilayani Misungwi,Mkoa wa Mwanza.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na bvaadhi ya watoto waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa Shule ya Msingi Ntulya,katika kata ya Mondo,wilayani Misungwi.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amembeba motto Paulo Muhangwa muda mfupi baada ya kuzindua shule ya Msingi Ntulya wilayani Misungwi,Mkoani Mwanza.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalmiana na baadhi ya wauguzi katika hospitali ya wilaya ya Misungwi wakati wa uzinduzi wa huduma ya X Ray katika hospitali hiyo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisiliza maelezo ya huduma ya Xray kutoka kwa mganga Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Dr.Marco Mwita Magessa muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua huduma hiyo katika hospitali ya Wilaya ya Misungwi.

MWANZA, Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kazi kuu na kipimo halisi cha kiongozi bora na hodari ni jinsi kiongozi anavyohangaikia maendeleo ya wananchi, ubunifu wake wa kuwaongezea wananchi mapato na kujali kumaliza kero zao.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa kazi ya madiwani nchini haiwezi kuwa ni kupokea posho za vikao ama kupima na kujigawia viwanja bali iwe ni kupambana na umasikini wa wananchi ambayo ndiyo kazi waliyoomba wakati wanatafuta kura za kuwa madiwani.

Vile vile, Rais amewataka madiwani wote nchini kutumia haraka na ipasavyo fedha zinazotolewa kwa ajili ya ujenzi wa barabara ndani ya halmashauri zao na siyo kuziweka hadi mwisho wa mwaka wa fedha na kulazimika kuzirudisha kwenye Mfuko wa Barabara.

Rais Kikwete ameyasema hayo wakati alipopokea Taarifa ya Maendeleo ya Wilaya ya Misungwi wakati alipoanza ziara ya siku tano katika Mkoa wa Mwanza kukagua na kufungua shughuli na miradi ya maendeleo.

                                         Akiuliza maswali na kutoa maelekezo wakati Ripoti hiyo inawakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Bibi Mariam Lugaija kwenye Shule ya Sekondari ya Misungwi, Rais Kikwete amewaambia viongozi wa Wilaya hiyo na wa Mkoa wa Mwanza:

“Kazi muhimu na uhodari wa kiongozi unathibitishwa na jinsi kiongozi huyo anavyopambana kupunguza umasikini wa wananchi na anavyobuni mbinu za kuongeza mapato ya wale anaowaongoza.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Kila kiongozi lazima awe na uchungu wa maendeleo na tamaa ya kuleta mabadiliko kwa wananchi wao. Kazi ya kiongozi ni kuhangaika na maendeleo ya wananchi.”

Akionyeshwa kutoridhishwa na kiwango cha uongozi cha baadhi ya madiwani mkoani humo, Rais Kikwete amewaambia viongozi hao: “Kazi ya madiwani haiwezi kuwa kupima na kugawa viwanja. Mliomba kazi ya udiwani ili kuwatumia wananchi na kuwaletea maendeleo. Nyie madiwani hamuwezi kuendelea kuwasibiri TASAF kuwaletea wananchi wenu maendeleo. Hii ni kazi yenu.”
Ameongeza kuelekeza Rais Kikwete: “Kazi yenu haiwezi kuwa ni kusubiri posho ya vikao na kupokea mishahara bure. Lazima muwe na tamaa ya maendeleo ya wananchi wenu.”
Aidha, aliwakumbusha kuwa Serikali inatoa fedha nyingi kwa halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwenye halmashauri hizo, lakini madiwani wanashindwa ama kuchelewa kuzitumia fedha hizo kujenga barabara hadi mwaka wa fedha unamalizika.

“Hili nalo halikubaliki. Kwa sababu Serikali inawapa fedha nyingi, lakini nyie hamzitumii kwa wakati na fedha hizo zinarudishwa kwenye Mfuko wa Barabara.”

No comments:

Post a Comment

Pages