HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

November 02, 2026

TEMBOCARD KUTOA ZAWADI ZA MILIONI 10 KWA WASHINDI WANANE

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


BENKI ya CRDB imezindua kampeni ya miezi mitatu ya Kila Mtu Apate na TemboCard, inayolenga kuwazawadia wateja wanaotumia kadi hizo kufanya manunuzi katika vituo vya mauzo na mitandaoni, ambapo washindi wanane watajinyakulia Sh milioni 10 kila mmoja.



Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Utumishi wa Benki ya CRDB, Godfrey Rutasingwa, amesema kampeni hiyo inalenga kuongeza hamasa ya matumizi ya TemboCard huku ikiwapa wateja nafasi ya kupata zawadi mbalimbali kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.


Amesema kampeni hiyo itadumu kwa miezi mitatu, kuanzia Oktoba 31, 2026 hadi Januari 31, 2027, ambapo wateja watakaotumia TemboCard kufanya manunuzi kupitia vituo vya mauzo (POS) au mitandaoni watakuwa na nafasi ya kushinda zawadi.


No comments:

Post a Comment

Pages