Na Elizabeth John
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Suma Mnazareti, anatarajia kuachia kibao chake kipya kitakachokwenda kwa jina la ‘Umechelewa’ hivi karibuni ambapo itakua ni muendelezo wa kuwapa buridani mashabiki wake.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Suma alisema katika kibao hicho ameshirikiana na msanii chipukizi ambaye anafanya vizuri katika tasnia ya muziki huo, Richard.
“Unajua kila msanii ana mashabiki wake hivyo naamini kutokana na kufanya kazi na msanii huyo, nina imani kibao changu kitapokelewa vizuri na mashabiki wa tasnia ya muziki huo,” alisema Suma Mnazareti.
“Nashukuru kazi zangu zinapokelewa vizuri na mashabiki, kitu ambacho kinaniongezea uwezo wa kuendelea kuandaa kazi nyingi ili kuendelea kufurahisha jamii pamoja na kuielimisha kupitia fani hii,” alisema.
Alisema amekuwa akiumiza kichwa kila siku kwa ajili ya kutengeneza vitu vizuri vyenye ujumbe kwa jamii, lengo lake likiwa ni kutoka kimaisha kupitia muziki.
No comments:
Post a Comment