HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 13, 2013

Tajiri Ng’ombe amuweka Kinyumba Mwanafunzi

Ø  Mwalimu Mkuu, Mwenyekiti wadai hali hiyo ipo kijijini hapo.
MWANAFUNZI wa Kidato cha Kwanza Jina linahifadhiwa wa Sekondari ya Mpwayungu, Kata hiyo Manispaa ya Chanmwino Dodoma, anadaiwa kuwekwa Kinyumba na Tajiri Ng’ombe, Faru Mwiliko na kumficha mahali pasipojulikana.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hii umbebaini kuwa Mwanafunzi huyo ni miongoni mwa wanafunzi wanne wanaodaiwa kuacha shule kutokana na tuhuma za kuwa na Ujauzito, Yudith Paulo Chigalamaso, (Form Four), Mariam Gabriel Masanjira (Form Three), Secelela Mnyampala (Form One), na Nyemo Chilongani (Form Two).

Hata hivyo katika hali ya kushangaza hakuna hatua zozote zilizoelezwa kuchukuliwa na Serikali ya Kijiji wakishrikiana na Walimu wa Sekondari hiyo. Lakini Mwalimu Mkuu, Andrew Honya, alikiri kuwepo kwa matukio hayo ila aliomba muda kwa kuwa alikuwa kwenye kikao.

“Ni kweli hali hiyo ipo, lakini niko kwenye majukumu ya ki-kazi mkoani Dodoma, na mahali nilipo siwezi kutoa maelezo yoyote, ila naahidi kutoa maelezo baada ya kukamilisha shughuli iliyopo mbele yangu hala tuzungumze”.alisema Honya.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji, Gabriel Hoya, wakiwa na Mtendaji wa Kijiji alimwambia Mwandishi hali hiyo ya wanafunzi kupewa Mimba na kuachishwa shule ipo lakini hakutoa maelezo nini utakuwa ufumbuzi wa kukomesha tabia hiyo.

Jitihada za kumpata Ofisa Elimu wa Shule za Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Dodoma, zinaendelea ili kujua hatua zitakazochukuliwa baada ya wanafunzi hao kukatishwa masomo, ukizingatia ni hivi karibuni mwalimu mmoja wa shule ya Msingi Sokoine, Davidi Macha (30) alikiri kumuweka kinyumba binti wa miaka 14.

Aidha baadhi ya Walimu waliohojiwa Shuleni hapo na kuomba majina yao yasitajwe walisema, Serikali ya Kijiji na hasa Viongozi akiwemo Mwenyekiti Hoya na Mtendaji wake, waliwatuhumu kwa kutokuwa na msaada kwa Wanafunzi hao, kwa sababu walishindwa kumsaidia Mwalimu aliyeibiwa Vitu vyake vyote na Mtu ambaye Kijiji kinamkumbatia.

No comments:

Post a Comment

Pages