HABARI MSETO (HEADER)


November 27, 2013

Solly Mahlangu kutumbuiza Tamasha la Krismas
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akifafanua jambo wakati akimtangaza  mwimbaji nguli wa nyimbo za injili kutoka Afrika Kusini, Solly Mahlangu ‘Obrigado’ambaye atashiriki katika tamasha la Krismasi 2013. 
 Msama akizungumza. Wa pili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi Abihudi Mang’era, Katibu wa kamati ya maandalizi Hudson Kamoga na Kulia ni Mussa Mkama mjumbe pamoja na Sunday Singa.
Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama, akifafanua jambo.
 Katibu wa kamati ya maandalizi Hudson Kamoga akizungumza.

 Na Mwandishi Wetu

WAKATI Tamasha la Krismasi likikaribia, muimbaji nguli wa muziki wa Injili wa Afrika Kusini, Solly Mahlangu ‘Obrigado’ni mmoja wa waimbaji ambaye anatarajia kuimba kwenye tamasha la Krismasi linalotarajia kuanza Desemba 25 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama mwimbaji huyo ataimba live siku hiyo pamoja na waimbaji wake wengine 14.

Msama alisema mwimbaji huyo anatarajia kushiriki katika tamasha hilo jijini Dar es Salaam, tamasha ambalo litafanyika pia katika mikoa ya Morogoro (26), Tanga (28), Arush(29) na Dodoma (1). 

Aidha Msama alisema bado wanaendelea kufanya mazungumzo na waimbaji wengine yameshakamilika kwa waimbaji wa ndani na nje ya Tanzania ikiwa ni pamoja, Solomon Mukubwa (Kenya), Ephraim Sekeleti (Zambia), Liliane Kabaganza (Rwanda).

Waimbaji wa Tanzania ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Edson Mwasabwite, New Life Band na John Lissu.

No comments:

Post a Comment

Pages