HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 02, 2013

Askofu Mshana; Msimseme Yesu mdomoni
 Familia zilizobariki watoto Mshoto mwenye Suti Nyeusi ni Mchungaji Naftari Njavike wa KKKT Mnadani Dodoma.
Kwaya Paradiso Mnadani KKKT ikionyesha Umahiri wa Uimbaji.

Na Bryceson Mathias, Mnadani Dodoma


WAKRISTO kote nchini, wametakiwa kutomsema Yesu Kristo mdomoni na badala yake wamthibishe na kumsema kwa Mawazo, Maneno na Matendo moyoni mwao, kwa sababu ni hakika Yesu anakuja kama alivyoahidi asitukute tunatangatanga.

Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Samweli Mshana, katika Ibada ya Sakramenti ya Kipa Imara iliyofanyika Usharika wa Mnadani, Jimbo la Makao, ambapo wahitimu 33 walibarikiwa.

Akihubiri katika Ubarikio huo Jumapili iliyopita [Desemba 1, 2013], Mshana aliwatahadharisha Wakristo kwamba, hawana sababu ya kumtaja Yesu midomoni mwao tu, bali wamdhihirishe mioyoni mwao kwa Mawazo, Maneno na Matendo, kwa kuwa ni hakika Yesu anakuja kama alivyosema.

“Ni Ukweli usiopingika Dalili zote za kurudi kwake zionekana kama alivyosema, hivyo hatuna sababu ya kuwa kama watu tusiojua alichosema, bali tunatakiwa kukaza macho na mioyo yetu kwake, ili tuje tumraki mawinguni tufurahi naye”.alisema Askofu Mshana.

Alilionya Kanisa (Waumini) na Wazazi na Taifa kwamba, Watoto wetu wa sasa hivi wanajua mambo mengi kuliko enzi yao kwa sababu ya Changamoto za Ki-Utandawazi, hivyo akatoa wito Kanisa, Wazazi, Jamii na Viongozi wa Taifa kutobweteka ila waombe kizazi hiki kisiharibiwe.

Mbali na Ibada ya Kipa Imara, Askofu Mshana alichangisha Shilingi Milioni 1.4/= kwa ajili ya Ujenzi wa Hostel ya Usharika huo (KKKT Mnadani) unaoongozwa na Mchungaji Naftari Njavike, Hostel ambayo ilikuwa imesimama kwa miaka kadhaa ili kupisha shughuli zingine za maendeleo, lakini kwa sasa ipo kwenye Lenta.

Kwa upande wake Mchungaji Kiongozi wa Usharika huo (Njavike), alimshukuru Askofu Mshana, Wazazi wa waliobarikiwa, Baraza la Wazee, Waumini na Watoto hao, kwa kufanikisha kuongeza Idadi ya Wakristo wapya yakiwemo Mafanikio ya Harambee ya Ujenzi wa Hostel.

Ibada hiyo ilihudhuriwa na Wachungaji wa Jimbo la Makao Makuu, Watumishi na Watendaji wote wa Dayosisi ya Dodoma, ambapo ilinogeshwa na Kwaya ya Usharika Mnadani na ya Paradiso, ambazo zilitumbuiza na kuboresha Sherehe Ibada hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages