Rais wa Blue Sky Media, Richard Signeski akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu ushirikiano walioingia na Kampuni ya Status Communication ya kuwawezesha waandaaji kuuza filamu kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii. (Picha na Francis Dande)
Omary Salisbury (kulia), akizungumza na waandishi wa habari.
Na Elizabeth John
KAMPUNI ya Status Communication imetangaza
kushirikiana na kampuni ya usambazaji wa filamu ya Kimarekani, Blue Sky Media
ili kuwawezesha waandaaji kuuza filamu kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.
Baadhi ya mitandao ambayo itatumika kusambaza
filamu hizo ni ITunes, Microsoft, You Tube, RAIN na mitandao mingine ya
kimataifa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi wa Blue Sky, Richard Signeski, alisema ushirikiano huu utawafanya
watengeneza filamu kutoka Afrika Mashariki na Kati kuweza kuuza filamu moja kwa
moja kwenye mitandao mikubwa ya usambazaji Dunia nzima.
“Lengo la ushirikiano huu ni kuwapa watengeneza filamu kutoka nchi hizo kuweza
kuuza filamu zao moja kwa moja kwa watazamaji Dunia nzima,” alisema.
Alisema wameamua kuja Tanzania baada ya kugundua
kwamba hapa kuna watengeneza filamu wengi wanahofia kuwekeza fedha nyingi
kwenye utengenezaji wa filamu zao kwani wengi wanahofia uchache wa masoko ya
kuuza filamu zao.
“Watengeneza filamu za hapa nchini, nawaomba
watengeneze filamu mjitokeze kwa wingi ili muweze kuuza filamu dunia nzima kwa
urahisi,” alisema Signeski.
Naye Mwakilishi wa Status Communication,
Monalisa Shayo, alisema ushirikiano wao na Blue Sky ni moja ya ushirikiano na kampuni
ya Kimataifa wanaotaka kuingia katika soko la Afrika Mashariki na Kati.
“Mwaka huu umekuwa na neema kwetu kwani tumeweza
kuingia mkataba na makampuni mbalimbali ili kuweza kuingia soko la Afrika
Mashariki, fursa hii ni muhimu kwa watengeneza filamu wan chi hizi kuuza filamu
kwenye masoko tofauti.
No comments:
Post a Comment