HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 16, 2013

HARAMBEE YA UMOJA WA VIJANA, UVCCM OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALLAM
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akisalimina na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya matembezi ya Vijana, Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum Machano Othman Said,mara alipowasili katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi, Oysterbay Jijini Dar es Salaam,leo katika hafla ya harambee ya kuchangia Jumuiya ya UVCCM kufanikisha Matembezi,ya vijana yanayoandaliwa na UVCCM Zanzibar. (Picha na Ramadhan Othman,Ikulu)
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,(katikati) akifuatana na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa,Sadifa Juma Khamis,(kulia) baada ya kuwasili  katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
  Miongoni mwa viongozi wa Jumuiya ya Chama cha Mapinduzi,katika UVCCM Octarian Msitiu, alipokuwa kichangia Shilingi za Kitanzania Miliioni Moja na Laki mbili,wakati wa Harambee ya kuchangia matembezi ya Vijana, yanayoandaliwa na UVCCM Zanzibar.
 Kada wa CCM Ramadhan Simai Makame, (Msheli) alipokuwa akichangia shillingi za Kitanzania Millioni mbili.
  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,akitoa tamko lake  la kuichangia Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM,(UVCCM) katika hafla ya Harambee kufanikisha matembezi katika maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,iliyofanyika leo katika Bwalo la Maafisa wa Polisi,Oysterbay Jijini Dar es Salaam,(kulia) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa,Sadifa Juma Khamis,(kushoto) akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,alipokuwa akizungumza na viongozi wa Umoja wa Vijana UVCCM,katika hafla maalum ya harambee kuchangia jumuiya hiyo katika kufanikisha matembezi ya Maadhimisho miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Pages