HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 07, 2014


DULLAYO ANASIKIA 'MAKELELE'
Na Elizabeth John
BAADA ya kutamba na ngomayake ya ‘Hawalali’, msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Abrahaman Kassembe 'Dullayo' amesambaza kazi yake mpya inayojulikana kwa jina la 'Makelele'. 

Mbali na kazi hizo, Dullayo alishawahi kutamba na ngoma yake ya ‘Twende na Mimi’ ambayo ilimtambulisha zaidi kuliko zote alizowahi kutoa kutokana na ubora wa mashairi yaliyopo ndani yake.

Akizungumza  jijini Dar es Salaam jana, Dullayo alisema ameamua kuachia kazi hiyo kwaajili ya kufungua mwaka pamoja na mashabiki wa kazi zake.

“Naomba sapoti kutoka kwa mashabiki wangu ili waweze kuipokea kazi hiyo ambayo naamini itakuwa moto wa kuotea mbali, kutokana na mpangilio mzuri wa mashairi, pamoja na kutaka kuuanza vizuri mwaka,” alisema Dullayo. 

Alisema anaamini kazi hiyo itafanya vizuri katika avituo mbalimbali vya redio kutokana na jinsi wimbo ulivyotengenezwa ikiwa ni pamoja na maandalizi aliyoyafanya.

“Mbali na kutaka kufungua nayo mwaka pia ni zawadi kwa mashabiki wangu kwani ni muda mrefu sijachaachia kazi hivyo naamini kupitia kazi hii nitaendelea kupata mashabiki mbalimbali,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages