HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 08, 2014

SERIKALI YATAKIWA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA
Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imeshauriwa kuboresha huduma mbalimbali katika hospitali zake nchini ili kupunguza vifo vya  mama wajawazito  na watoto chini ya miaka mitano  vinavyotokana ukosefu wa vifaatiba.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaami,  Brigedia Mstaafu, Haroun Othman wakati wa sherehe za kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014, zilizoandaliwa na wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Vijibweni, Kigamboni jijini.

Alitaja baadhi ya mahitaji kuwa ni uhaba wa dawa, vifaatiba pamoja na madaktari, wauguzi na hata mazingira ya wafanyakazi nayo sio mazuri kiutendaji.

“Pamoja na changamoto mbalimbali zinazochangiwa na mazingira magumu bado hospitali hii yaVijibweni inatoa huduma nzuri na kwa ufanisi wa hali ya juu jambo linaloifanya ijivunie mafanikio yake tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006,”alisema Othman.

Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu na wafanyakazi, Dk Alfred Mchinamnamba, alisema hospitali hiyo imekuwa ikiendelea na mpangomkakati wa kutoa huduma bora kwa wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo.

Aliongeza kuwa kwa wale wanaohitaji matibabu zaidi hupelekwa katika hospitali ya wilaya Temeke ama katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Aidha, Mchinamnamba, aliwaomba baadhi ya wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo, wakati mwingine wawe wavumilivu kutokana na changamoto wanazokumbana nazo kwani nyingine zinasababishwa na idadi ndogo ya wafanyakazi.

No comments:

Post a Comment

Pages