MKUTANO Mkuu wa kujadili
changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara ikiwemo mfumo mbaya wa
uendeshaji biashara nchini, unafanyika
jijini Dar es Salaam Januari 9.
Katibu wa Umoja wa
Wafanyabiashara Kariakoo, Sued Chemchem, alisema mkutano huo utawakutanisha
viongozi wa wafanyabiashara kutoka mikoa yote ya Jamhuri ya Muungano, ambako
unatarajiwa kuanza saa tatu asubuhu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini.
Alisema mkutano huo utajikita
zaidi kujadili na kuandaa utaratibu ambao utaleta tija kwa ajili ya wafanyabiashara
hao nchini.
Chemchem alisema miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa leo ni
pamoja na uchaguzi wa wajumbe ambao wataunda tume yao kwa ajili ya kukutana na
wataalam wa Wizara ya Fedha, Biashara na Viwana na wale wa TRA.
Alisema lengo la kukutana na
wataalamu hao ni kutaka kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali
zinazojitokeza hususan matumizi ya mashine ya kutolea stakabadhi (EFD).
‘Tunatarajia mgeni rasmi
atakuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Abdallah Kigoda kama tulivyomuomba.
“Huu ni mkutano muhimu na
ndio mana tunawataka wafanyabiashara wote wafike, hakuna atakayefunga duka
kwani kila duka linazaidi ya watu wawili, kwa wale wasio kuwa na wasaidizi
watapima wenye umuhimu wa mkutano huo;”alisema Chemchem.
Hata hivyo baadhi ya wakazi
wa jiji la Dar es Salaam wameingiwa na hofu kuwa huenda wafanyabiashara hao
wasifungue maduka kwa ajili ya mkutano huo waliouita muhimu kuliko mambo yote.
No comments:
Post a Comment