HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 01, 2014

TASWA FC YAANZA MWAKA MPYA KWA KUICHAPA TWANGA PEPETA 1-0
 Beki wa timu ya Taswa Fc Sufianimafoto (kulia) akiwania mpira na mshambuliaji wa Twanga Fc, wakati wa mchezo wa kirafiki wa Bonanza la kufunga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya wa 2014, lililofanyika kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, leo jioni. Katika mchezo huo Taswa ilianza mwaka mpya kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Juma Pinto katika kipindi cha pili.
 Mshambuliaji wa Taswa Fc, Juma Pinto (katikati) akiwatoka mabeki wa Twanga Pepeta Fc, wakati wa mchezo huo.
 Beki wa Taswa Fc, Athuman (kulia) akiwatoka wachezaji wa Twanga Pepeta.
 Winga wa Taswa Fc, Zahro Milanzi (kulia) akimiliki mpira......
 Kocha wa Twanga Pepeta Fc, ambaye pia ni Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka, akitoa mawaidha kwa wachezaji wake wakati wa muda wa mapumziko.
 Wachezaji wa Taswa Fc, wakimsikiliza Kocha mchezaji Ally Mkongwe, wakati wa mapumziko.
 Benchi la Twanga likiwa haliamini kilichotokea uwanjani...
 Hapa utaenda wewe mpira utabaki.........tulia kama ulivyooooo.....
 Hapiti mtu hapa........
 Mwamuzi wa mchezo huo akichezesha huku akiwa na chupa ya soda ya Novida iliyo na kinywaji cha Konyagi ndani yake......

No comments:

Post a Comment

Pages