HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 07, 2014

TCAA YAAJIRI WAKAGUZI WA MARUBANI
Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) wakitoa maelezo kuhusu shughuli wanazozifanya walipotembelewa na wananchi mbalimbali waliohudhuria maonyesho ya kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika kwenye viwanja vya Betrasi mjini Unguja.

Na Irene Mark, Zanzibar

KATIKA  kukabiliana na uhaba wa Wakaguzi wa Marubani wa Ndege, Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) imeajiri wataalam watatu wa kada hiyo kwa mwaka 2013.

Ofisa Habari wa Mamlaka hiyo, Ally Changwila alisema kuwa kuajiriwa kwa wataalam hao kunaongeza idadi yao na kufikia sita kwa sasa.

Ofisa huyo alisema hayo wakati wa maonyesho ya siku tatu ya kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar yaliyomalizika jana visiwani humo.

Kwa mujibu wa Changwila kada hiyo ya wakaguzi wa marubani inakabiliwa na upungufu wa watumishi 12 ili kufanikisha ufanisi katika eneo hilo.

Aliongeza kwamba changamoto mbalimbali zinachangia eneo hilo kuwa na watumishi wachache ni gharama kubwa za masomo ya kada hiyo nje ya nchi na uduni wa mishahara.

Awali alibainisha kwamba mwaka 2013 katika upande wa usajili wa ndege TCAA imesajili helkopta tatu mpya ambazo sasa zinatumika kufanikisha shughuli za utafiti wa mafuta, gesi na huduma za kukodi.

Alieleza majukumu muhimu ya mamlaka hiyo kuwa ni udhibiti wa usalama, udhibiti uchumi katika eneo la anga na utoaji wa huduma za uongozaji wa ndege.

No comments:

Post a Comment

Pages