Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya Hamis Mdee akipima afya yake
kwenye banda ya NHIF katika maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi
Zanzibar.
Mwakilisho wa NHIF Zanzibar Ismail Kangeta
(Katikati) akitoa elimu ya umuhimu na namna ya kujiunga na Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya katika maonesho hayo.
Ofisa Elimu kwa Umma wa NHIF, Grace Michael
akifafanua jambo kwa wananchi waliofika katika banda la Mfuko huo.
Wananchi wakiendelea kupata huduma ya kupima
afya zao ikiwemo uzito na hatimaye kupata elimu ya kujikinga na maradhi
yasiyoambukiza.
Ofisa wa NHIF katika ofisi ya Zanzibar, Shaaban
Mhunzi akitoa huduma kwa wananchi waliofika bandani hapo.
Bi. Asha Alli akipima sukari na kupata ushauri
wa kitaalam kutoka kwa mtaalam Khamis Haji Haji.
Kaimu Mkurugwenzi Mkuu wa NHIF, Hamis Mdee
akibadilishana mawazo na mwakilishi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam
Dennis Madaha wakati wa maonesho hayo.
Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma Catherine Kameka
akitoa elimu kwa wananchi waliofika bandani hapo. (PICHA ZOTE NA IDARA YA MASOKO NA ELIMU KWA UMMA NHIF)
Na Irene
Mark, aliyekuwa Zanzibar
VIJANA wengi
wenye umri kati ya miaka 30 na 40 wanakabiliwa na tatizo la uzito uliozidi hali
inayowaweka kwenye hatari ya kupata magonjwa yasiayoambukizwa.
Akizungumza wakati wa maonyesho ya kuadhimisha miaka 50 ya Mapunduzi Zanzibar, Ofisa
Uhakiki Ubora wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Dk. Ally Mvita alisema
hiyo ni hatari kwa taifa.
Kwa mujibu
wa Dk. Mvita magonjwa yasiyoambukizwa yanayotokana na uzito wa mwili kuzidi ni
Kisukari na Shinikizo la Damu ambayo hudhoofisha nguvukazi ya mgonjwa na
kuzorotesha maendeleo binafsi na taifa.
“Katika
kipindi cha siku nne za maonyesho haya tumewapima bure wananchi zaidi ya 700
wengi ni vijana wenye umri kati ya miaka 30 na 40 ambao asilimia zaidi ya 75 ya
vijana hao tumegundua kwamba wanauzito uliozidi.
“Kitaalam
tunaita ‘over weight’ na ‘obesity’ uwiano wa urefu na uzito kiafya havilingani,
hii ni hatari kwa sababu ni rahisi mtu huyo kupata kisukari na shinikizo la
damu,” alisema Dk. Mvita.
Aidha
aliwashauri watu wenye matatizo hayo kufanya mazoezi na kupunguza ulaji wa
vyakula bila mpangilio ili kujiepusha na magonjwa hayo.
Maonyesho
hayo yalimalizika Januari 5 mwaka huu kwenye viwanja vya Betras, mjini Unguja
ambapo viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi (SMZ) na ile ya Muungano
walitembelea banda la NHIF na kupima afya zao.
No comments:
Post a Comment