Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Inspekta Isack Lema Mlezi wa Bodaboda Mkoa wa Mbeya kwa upande wa jeshi la Polisi wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Mtenda uliopo Soweto mjini Mbeya kwa ajili ya kuzungumza na waendesha Bodaboda wa mjini Mbeya, ambapo wamemweleza matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo na jinsi wanavyoshirikiana na jeshi la polisi na polisi jamii katika kulinda usalama wa wananchi, wao wenyewe na mali kwa ujumla, Chanagamoto mbalimbali za kimaendeleo zimetatuliwa na zitaendelea kutatuliwa ili waendesha bodaboda wafanye kazi zao kwa ufanisi na utulivu. (Picha na Fullshangwe-Mbeya)
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia waendesha Bodaboda ambao wameonekana kufurahia sana mkutano huo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa mtenda Soweto jijini Mbeya.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Blogger wa Mbeya yetu Blog Bwana
Joseph Mwaisango.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha ya pamoja na uongozi wa waendesha Bodaboda kushoto ni mwenyekiti Vicent Mwashoma na kulia ni Msumba Makya Katibu wa Waendesha Bodaboda
No comments:
Post a Comment