HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 28, 2014


MAELFU WAJITOKEZA KUUGA MWILI WA ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA MARA MAREHEMU JOHN GABRIEL TUPA
Na Shomari Binda, Mara
MAELFU ya wananchi wa mkoa wa Mara pamoja na mikoa jirani wakiongozwa na viongozi wa Serikali, Dini na vyama vya Siasa wameuaga mwili wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara John Gabriel Tupa aliyefariki juzi asubuhi akiwa wilayaniTarime kwa shughuli za kikazi.

Akitoa salamu za rambirambi za Serikali mkoani Mara, Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Mara Bartazal Kichinda alisema walipokea kwa masikitiko makubwa msiba wa ghafla wa mkuu wa mkoa wa Mara John Gabriel Tupa  kwa kuwa msiba huo umekuja wakati mchango  na usaidizi wa kiongozi huyo ukiwa unahitajika zaidi mkoani Mara.
 Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa mara, John Gabriel Tupa ukitolewa kwenye makazi yake. (Picha kwa Hisani ya Shomari Binda)
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa.
 Baadhi ya waombolezaji.


 Kutoka kushoto ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Paul Kasabago, Christopher Gachuma.
 Mwenyekiti wa Bakwata, Musoma mjini akiwa na Askofu Msonganzila wa Kanisa Katoliki.
 Rais wa kklabu za waandishi wa habari, Keneth Simbeya akitoa salama za rambirambi.
 Mtoto wa marehemu akitoa shukrani kwa watu waliofika kuwafariji wakati wa msiba.
 Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akiwa na waombolezaji wengine.
 Askofu Msonganzila akiweka sahihi kwenye kitabu cha waombolezaji.
Askofu Msonganzila akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa marehemu.
 Baadhi ya waandishi wakipita mbele ya Jeneza la marehemu weakati wa kuaga mwili. Bigambo Jeje (mbele)
 Waombolezaji.

 Mkurugenzi wa klabu za waandishi wa habari Tanzania, abubakari Karsan (kulia), nyuma yake ni Madaraka nyerere wakitoa heshima za mwisho.

 MGENDI WA CHANEL TEN AKIWAJIBIKA KUWAPA WATANZANIA TAARIFA
 Baadhi wanafunzi wakipita kutoka heshima za mwisho.
 NAMI NILIMUAGA MKUU WA MKOA JOHN TUPA,KWA KWELI NI PIGO

 Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara ukitoka kwenye makazi yake kwa ajili ya safari ya kwenda kanisani.
 Mwili wa marehemu ukiwasili kanisani.
 Mke wa marehemu John Tupa (wa pili kushoto), akiwa na wanafamilia.

No comments:

Post a Comment

Pages