Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro, Amio T. Amio (kushoto) akisalimiana na wafanyakazi wa Benki ya Exim wakati wa Mbio za Riadha za Ngorongoro zilizofanyika kupiga vita ugonjwa wa Malaria. (Na Mpiga Picha Wetu)
Mkurugenzi wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Amio T. Amio (kushoto) akikabiziwa zawadi ya kava la tairi ya gari kutoka kwa Ofisa Mauzo wa Benki ya Exim tawi la Karatu Nectae Exaud wakati wa Mbio za Riadha za Ngorongoro zilizofanyika kupiga vita ugonjwa wa Malaria.
Mratibu - Ufundi wa Mbio za Riadha za Ngorongoro wa kwanza kulia Filbert Bayi akitoa maelezo kwa wakimbiaji. Wa kwanza kushoto aliyevaa miwani ni Meneja wa Benki ya Exim tawi la Karatu Emmanuel A. Mwamkinga. Mbio hizo zilifanyika kupiga vita ugonjwa wa Malaria nchini.
Wafanyakazi wa Benki ya Exim wakiwa na medali zao baada ya kukabiziwa medali hizo wakati wa Mbio za Riadha za Ngorongoro zilizofanyika kupiga vita ugonjwa wa Malaria.
Wafanyakazi wa Benki ya Exim wakiwa na medali zao baada ya kukabidhiwa medali hizo wakati wa Mbio za Riadha za Ngorongoro zilizofanyika kupiga vita ugonjwa wa Malaria.
Na Mwandishi Wetu, Karatu
Benki ya Exim imejikita katika kusaidia maendeleo ya michezo
nchini hususani mchezo wa riadha, ambao kwa siku za nyuma umekuwa ukipeperusha
bendera ya Tanzania dhidi ya mataifa mengine ipasavyo katika mashindano ya
kimataifa.
Ikiwa ni Benki
ya sita kwa ukubwa Tanzania kwa upande wa mali na amana
zake, Benki ya Exim imesema kwamba inataka kuwa sehemu
ya mkakati wa heshima hiyo iliyopotea, ambapo imeanza kuingiza misaada
yake katika michezo ya ngazi za chini ili kugundua
vipajivilivyojificha na kuweza kuvitumia.
Akizungumza wakati wa mbio za riadha za Ngorongoro
zilizoandaliwa na Zara Tanzania Adventures mwishoni mwa wiki mkoani
Kilimanjaro, Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Karatu, Bw. Emmanuel Mwamkinga
alisema kuwa kuunga mkono miradi mbali mbali ya kijamii nchini ni moja kati ya
shughuli za kijamii zinazofanywa na Benki ya Exim.
“Mbio hizi zitawezesha vipaji vyetu katika ngazi ya chini
kabisa kuonekana ambavyo upaswa kutumika ili kushiriki katika mashindano ya
kimataifa. Mpaka sasa kuna wasiwasi kuwa kwa nini wanariadha wa kitanzania
wanashindwa kuleta medali nyumbani, kinyume na ilivyo zamani. Kwa hivyo hii ni
fursa ya kipekee kwa Chama cha Riadha nchini kutambua wanariadha wazuri na
kuwaandaa vizuri ili waweze kuiwakilisha nchi kikamilifu,” alisema.
Bw. Mwamkinga alibainisha kuwa benki yake, kupitia tawi lake
la Karatu imeungana na wadhamini wengine kupiga jeki mbio hizo ambazo lengo
lake ni kuunga mkono jitihada za serikali za kukuza uelewa dhidi ya ugonjwa wa
malaria, na kutokana mbio hizo vipaji vipya katika riadha vitagundulika.
Pia alisema
kuwa udhamini huo ni moja kati ya mipango ya benki ikiwa
inaangalia uwezekano wa kupanua huduma zake mkoani Kilimanjarona kwamba
itakuwa ni fursa nzuri kwa benki kukuza jina lake.
"Benki ya
Exim inajivunia kudhamini mbio hizi za Ngorongoro na kujiusisha
nazo ambayo ni njia nzuri kwa watu kuifahamu benki ya Exim vizuri na
ni fursa ya kujiinua kibiashara.
"Ngorongoro Marathon ni tukio ambalo
linaumuhimu mkubwa katika kuitangaza Tanzania katika nyanja
nyingi hasa uwezo mkubwa wa kiuchumi wakati pia utoa fursa
kwa wanariadha wanaochipukia na wapya kupatikana,”
Bw. Mwamkinga alisema.
No comments:
Post a Comment