Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kwa vyombo vya habari na wananchi wote kwa ujumla
kuwa leo tarehe 13 April 2014 mnamo saa tatu na nusu asubuhi (3:30 Hrs),
kumetokea ajali ya Ndege ya JWTZ aina ya Helikopta katika Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Mwl Julius Kambarage Nyerere ( upande wa Jeshi). Helikopta hiyo
ilipata ajali ilipokuwa katika hatua ya kuanza kuruka.
Helikopta
hiyo ilikuwa imewabeba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe
Dr. Ghalib Bilal na ujumbe wake ambao ni Waziri wa Ujenzi; Mhe. Dr. John
Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Said Mecky Sadick na amishina Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum Kamishina Suleiman Kova.
Aidha,
Wengine waliokuwemo ni Dr. Mnzava, Msaidizi
wa Makamu wa Rais, Msaidizi wa Kamanda Kova na waandishi wa habari watatu.
Ujumbe
wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulikuwa katika safari ya kuzungukia maeneo yaliyo
athirika na mafuriko katika jiji la Dar
es Salaam na Mkoa wa Pwani kufuatia mvua kubwa iliyoanza kunyesha kuanzia
tarehe 11 April hadi sasa.
Makamu
wa Rais pamoja na ujumbe wake hawakupata majeraha katika ajali hiyo. Aidha,
rubani na wasaidizi wake pia wametoka salama.
Uchunguzi
wa ajali umeanza mara moja kwa ajili ya
kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Imetolewa na
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao Makuu ya
Jeshi, Upanga
SLP
9203, Simu: 0754270136
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment