HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 19, 2014

Jojo Walaani Wanaume na Wanawake kufungwa Chumba kimoja
Na Bryceson Mathias, Mbeya

WANANCHI wa Kijiji cha Jojo, Kata ya Santilya, Wilaya ya Mbeya vijijini, wamelaani kitendo cha Katibu Mtendaji wao, Anderson Yamalila, kuwakamata Wanaume Watano na Mwanamke mmoja na kuwafungia Chumba kimoja, akidai waligoma kufanya kazi za Maendeleo kijijini hapo.

Akifafanua tuhuma hizo baada ya Mtendaji huyo kutopatikana kupitia simu yake ya mkononi  07689503390Mwenyekiti Mwasile alikiri kuwepo kwa tukio hilo lililofanywa na Mtendaji wake wa kijiji na kudai walikuwa wamehifadhiwa kwenye Chumba ili hali yeye mwenyewe (Mwasile) akiwepo, na sababu ilikuwa ni kutokana na madai ya kukaidi kufanya shughuli za maendeleo kijijini humo.

“Ni kweli vijana hao walikamatwa na Mtendaji na kuwekwa kwenye Chumba kimoja cha Sebuleni kutokana na ukaidi wao wa kufanya shuguli za maendeleo, lakini hata mimi mwenyewe si kuwa mbali nilikuwepo”.alisema Mwasile.

Hata hivyo ilibainika Vijana hao waliokamatwa walitetewa na Wanaharakati na Vionngozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakimtahadharisha Mtendaji Yamalila kwamba, Sheria za nchi na za Haki za Binadamu, haziruhusu Jinsia hizo tofauti kufngwa chumba kimoja.

Kutokana na ubabe wa ukiukwaji huo, imedaiwa Mtendaji Yamalila aliamuru Askari Mgambo wawapiga vijana hao huku akiahidi kula sahani moja na Viongozi wa Chadema, akiahidi kuwabambikiza Kesi hadi awafunge, kwa maana wanamkosesha usingizi na kukiharibu Chama Tawala cha CCM.

Aidha Mzazi wa Kiongozi mmoja wa Chadema aliyejitambulisha kwa jina la Amani Mwasote (CCM) alionya akisema, yeye ni CCM lau mkewe na mwanae ni Chadema,

“Sifurahishwi na tabia ya Mtendaji Yamalila kuniambia niwaonye mke wangu na mwanangu warudi CCM kwa kuwalazimisha. Mtendaji afanye siasa za kistaarabu, asitumie nguvu ya Serikali vibaya kuwatisha Chadema ili kuwafurahisha wakubwa wake na kuwatesa watoto wetu”.alisema Mwasote   

No comments:

Post a Comment

Pages