Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi, katika kijiji cha Ilemba, kata ya Ilemba, alipohutubia wananchi katika kata hiyo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika wilaya Sumbawanga Vijijini mkoani Rukwa, leo Aprili 3, 2014. ©2014 theNkoromo Blog
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya watu, katika kijiji cha Ilemba, kata ya Ilemba, alipohutubia wananchi katika kata hiyo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika wilaya Sumbawanga Vijijini mkoani Rukwa, leo Aprili 3, 2014. ©2014 theNkoromo Blog
Maelfu ya wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo kwenye Kijiji cha Ilembo wilaya ya Sumbawanga Vijijini ©2014 theNkoromo Blog
Katika hali inayoonyesha wananchi wengi kuridhishwa na utendaji kazi wa Kinana, mmoja wa wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa kiongozi huyo katika kata ya Ilembo wilaya ya Sumbawanga Vijijini wakiwa na bango la kusifu uchapakazi huo wa Kinana
Kinana akimpa kadi ya CCM, mwanachama mpya Eva Thomas, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Ilemba, Sumbawanga Vijijini. Zaidi ya wanachama wapya 250 wa CCM, walikabidhiwa kadi
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Mjumbe wa NEC Balozi Ali Karume wakiingia kwenye Uwanja wa mkutano huo.
Vijana wa UVCCM wakiimba kwaya wakati wa mkutano wa Kinana, kijiji cha Ilemba
Kinana akifurahia vijana wakati wakicheza ngoma kumlaki alipowasili uwanja wa mkutano katika kata ya Ilembo
Kinana akisaidia kuweka dirisha kwenye bweni la wasichana shule ya sekondari, Ilembo Sumbawanga Vijijini wakati wa ziara yake katika wilaya hiyo.
Kinana akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Vijijini kwa kufanikisha usimamizi wa ilani ya CCM kwa kujenga bweni hilo la wanafunzi katika shule ya sekondari ya Kata ya Ilembo wilayani humo.
Kinana akishiriki ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Kata ya Ilemba, Sumbawanga Vijijini. Ameahidi kutoa mifuko 50 ya saruji na bati 50 kumalizia ujenzi wa kituo hicho
Kinana akifungua shina la wakereketwa la Vijana wa UVCCM la Makoko, katika Kijiji cha Ilemba
Kinana akizindua shina la Vijana la Makoto, Ilemba Sumbawanga Vijijini
Msafara wa Kinana ukipita kwenye mto kutokana daraja kuharibika katika barabara ya kutoka Kata ya Ilembo kwenda Sumbawanga mjini.
Wananchi wa Kijiji cha Milepa A wakimshangilia Kinana baada ya kusimamisha msafara wake wakati akitoka Kata ya Ilembo kwenda Sumbawanga mjini
Wananchi wa Kijiji cha Mtoisa, wakiwa wamesimamisha njiani msafara wa Kinana wakati akitoka Kata ya Ilembo kwenda Sumbawanga mjini
Vijana wa Kijiji cha Kalakala, Kata ya Muze wakisakata ngoma kumpokea Kinana alipowasili eneo hilo akiwa njiani kutoka Kata ya Ilembo kwenda Sumbawanga mjini
Wananchi wa Kijiji cha Kalakala, Kata ya Muze wilaya ya Sumbawanga Vijijini, wakimshangilia baada ya kutangaza kuchangia mifuko 100 ya saruji na bati 100 ujenzi wa zahanati ya Kata hiyo
Kinana akiwashukuru wananchi wa Kijiji cha, Kata ya Muze baada ya kumlazimisha kuzungumza nao licha ya kufika eneo lao saa moja jioni, wakati akitoka Kata ya Ilembo wilaya ya Sumbawanga Vijijini kwenda Sumbawanga mjini.©2014 theNkoromo Blog
Mkazi wa Kijiji cha Muze akinyonyesha mtoto wake wakati akiwa miongoni mwa wananchi wa kijiji hicho waliomlaki Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alipowasili kwenye kijiji hicho akiwa njiani kutoka Kata ya Ilembo, Sumbawanga Vijijini kwenda Sumbawanga mjini leo, Aprili 3, 2014. Picha zote na Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog
No comments:
Post a Comment