Kutokana na kukithiri kwa mfumo dume
unaoambatana na ukandamizaji wa mwanamke na kusababisha ongezeko la watoto
yatima na wajane katika jamii ya wafuagaji wa kimasai, wanawake wa jamii hiyo wanaoishi ndani ya eneo la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro
wameunda baraza la wanawake litakalosimamia masuala mbalimbali kwa mtoto
wa kike husani elimu,afya,na haki ya mwanamke.
Wanawake hao wa jamii ya kimasai wanabainisha
kuwa hamasa ndogo ya jamii ya kuwasomesha watotot wa kilke na kutopewa
kipaumbele ,afya duni ya jamii hasa mama na motto endapo vitazingatiwa katika
jamii hiyo vitasaidia kuondokana na changamoto hizo na hatimae kuongeza idadi ya
wasomi hasa watoto wa kike ambao wataikomboa jamii hiyo kwa ujumla .
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza
hilo uliofanyika katika makao makuu ya
mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro ukienda sambamba na harambee ya kuchangia
mfuko wa elimu kwa watoto wa kike makamu
mwenyekiti wa baraza hilo bibi mereyo muresi anasema litakua chombo muhimu cha kuwasemea wanawake
katika vyombo vya maamuzi ndani na nje.
Mhifadhi mkuu wa mamlaka ya ngorongoro dakta
fredy manongi ndiye aliyezindua baraza hilo na kuendesha harambee
iliyofanikisha kupatikana kwa zaidi ya shilingi milioni sabini fedha taslimu na
ahadi.
Baraza la wanawake hao wafugaji linaanzishwa huku tayari kukiwa
na baraza la wafugaji ngorongoro ambalo mwenyekiti wa baraza hilo metui ole
shaudo anawaasa kuwa lengo
walilokusudia la kumkomboa mwanamke
litafikiwa kwa wao kushirikiana na wadau
wengine
No comments:
Post a Comment