HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 14, 2014

WATOA HUDUMA ZA KIJAMII WAPATA MAFUNZO YA LUGHA YA ALAMA


Na Joseph Malembeka Kilombero

ZAIDI ya watoa huduma za kijamii 50 wakiwemo askari polisi,walimu,wauguzi na madaktari wamepewa elimu ya lugha za alama kutoka katika tarafa mbili za Mlimba na Kidatu.

Akizungumza na mwandishi wa habri hizi mratibu wa mradi wa mafunzo ya alama wilayanihumo Elizabeth Rutha alisema mradi huo wenyelengo la kuwafikia wahudumu 137 umeanza na tarafa hizo na  baadae tarafa Mngeta na Ifakara.

Alisema mradi huo unaofdhiliwsa na Foundation for civil society wa mwaka unatarji klugharimu shilingi mil 42.7.

Amesema wameamua kutoa mafunzo hayo kwa sababu viziwi wengi wanapata tabu wawapo katika vituo vinavyotoa huduma za kijamii kutokana na kutokuwa na wataalamu wa lugha ya alama na wakalimani.

Kwa upande wao waliopewa mafunzo hayo wameipongeza Chavita Kilombero kwa kuwapa mafunzo hayo kwani awali walikuwa katika wakati mgumu wa kushindwa kuwasiliana na viziwi kwa kutokufahamu njia za mawasiliano na hali hiyo ilipelekea kuwasaidia pale watakapokuwepo wakalimani.

Hata hivyo wameomba mafunzo hayo yawe yanatolewa mara kwa mara ili wawe na uwelewa mpana zaidi wa kufahamu lugha ya alama ili kurahisisha mawasiliano baina ya pande hizo mbili  kwa lengo la kuwapatia huduma muhimu za kijamii kama wanazopata watu wasiokuwa na matatizo.

No comments:

Post a Comment

Pages