Na Bryceson Mathias, Santilya Mbeya
WANACHAMA zaidi ya 60 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kijiji
cha Jojo, Kata ya Santilya, Mbeya vijijini, kwa mwezi mmoja
sasa wametimka na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
kiasi cha kumtia hofu Mtendaji wa Kijijiji hicho na kutoa vitisho.
Mtendaji huyo, Anderson Yamaliha, alijikuta akitishika
na timka tika hiyo, iliyompelekea kutoa vitisho kwa waliohama kwamba warejee
kwenye Chama cha Mapinduzi (CCM) haraka iwezekanavyo na wasipofanya hivyo
watabambikiziwa kesi na kuchukuliwa hatua kali.
Mtendaji Yamaliha alipotafutwa kwenye simu 07689503390 ajibu
tuhuma zake, Simu ya Mlinzi huyo wa Amani hakujibu, na alipoandikiwa
Ujumbe Mfupi hakujibu ambapo Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Jojo, Nelson
Mwasile, alitoa ufafanuzi kuwa amepata malalamiko ya vitisho atayashughulikia.
“kuna taarifa kwamba ya kwamba vijana wa Chadema wamekataa
kufanya Shughuli za Maendeleo na kazi za kijiji, kulikopelekea wao kukamatwa na
Mtendaji na kudaiwa kuwa wamepigwa na Askari Mgambo na kudaiwa wametishiwa kubambikiziwa
kesi, nitawakutanisha na kumaliza mgogoro huo”.alisema Mwasila.
Vijana waliohamia Chadema na kujiunga na ‘Red Brigade’ ambao
wamechangia kuwafanya wanakijiji wengi wahame na kujiunge na Chadema, wameapa
hawawezi kurejea, na kuwataka wazazi wao wanaosumbuliwa na mtendaji huyo kuwa
warejee CMM, wampuuze.
Katibu wa Chadema Jojo, Osia Mwapepu amethibitisha kuwepo
Mgogoro wa kutoelewana na Vijana wake wa Chadema, na kumekuwa na vitisho
vinavyotolewa na Mtendaji wanaojiunga na Chama chake, ambapo alithibitisha
wanachama 60 hadi 100 CCM wamehamia Chadema, ila nao wamepoteza wanachama wanne
na Kiongozi mmoja.
No comments:
Post a Comment