Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Mbwana Mohamed Mb Dog (pichani), amesema baada ya kuachia video yake ya ‘Mbona Umenuna’, anaendelea na juhudi za kuwapatia raha wadau na mashabiki wake kama njia ya kuonyesha makali yake kisanaa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mb Dog alisema video yake imeandaliwa kwa kiwango
cha juu, huku ikiwa ni sababu ya yeye kuendelea kutoa nyimbo nzuri
zinazoonyesha ubora wake.
Alisema kuwa
lengo lake ni kufanya makubwa zaidi katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva,
hasa baada ya kuamua kurudi tena katika soko hilo kwa mikakati ya aina yake.
“Nipo katika
harakati za kuonyesha namna gani naweza kuonyesha ubora wangu kama ilivyokuwa
mwanzo nilipotoka na wimbo wa kwanza wa Latifa, nikiwa na ‘Madee’.
“Naamini hii
ni njia nzuri ya kuwapatia burudani kamili wadau na mashabiki wangu katika
tasnia ya muziki wa kizazi kipya, hasa baada ya kuachia video yangu ya Mbona
Umenuna,” alisema Mb Dog.
No comments:
Post a Comment