HABARI MSETO (HEADER)

Breaking

May 31, 2014

MKUTANO WA UKAWA USHIROMBO MKOANI KAGERA
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa, akihutubia mkutano wa hadhara huku mamia ya wananchi wakimuonesha vidole vitatu kuashiria wanataka Serikali Tatu ndani ya Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika Kijiji cha Namonge Wilaya ya Ushirombo mkoani Kagera juzi.  (Na Mpiga Picha Wetu).
 Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akisalimiana na wanafunzi wa Sekondari Namonge iliyopo Kijiji cha Namonge, Wilaya ya Ushirombo mkoani Kagera waliojitokeza barabarani karibu na shule hiyo kisha kuzuia msafara wake wakaati akielekea kwenye mkutano wa hadhara kijijini hapo juzi.
Umati wa watu wakiwa wamenyoosha mikono yao kukubaliana na muundo wa Serikali Tatu katika Katiba Mpya pamoja na kutorudi bungeni wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi hapo Agosti iwapo Serikali haitaamuru kujadiliwa Rasimu ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba, katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa mpira Ushirombo mkoani Kagera juzi.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akimvisha tisheti ya M4C ya chama hicho, Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Igulwa wilayani Ushirombo mkoani Kagera, Emmanuel Charles Ndatulu, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa mpira Ushirombo mjini baada ya kurudisha kadi ya CCM yeye na wengine 41 kisha kujiunga na Chadema juzi.
 Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Igulwa Wilaya ya Ushirombo mkoani Kagera, Emmanuel Charles Ndatulu (kushoto), akisoma moja ya kifungu cha Biblia baada ya kujiunga na Chadema kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa mpira Ushirombo mjini juzi.
Umati wa watu wakiwa wamenyoosha mikono yao kukubaliana na muundo wa Serikali Tatu katika Katiba Mpya pamoja na kutorudi bungeni wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi hapo Agosti iwapo Serikali haitaamuru kujadiliwa Rasimu ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba, katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa mpira Ushirombo mkoani Kagera juzi.

No comments:

Post a Comment

Pages