HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 10, 2014

NSSF YAPIMA AFYA BURE KWA WAKAZI WA MKOA GEITA
Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), linaendesha  kambi za upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa kanda ya ziwa kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Lengo la kambi hizi ni kuweza kutoa elimu na  kuwahamasisha wanachama wa NSSF na wananchi kwa ujumla waweze kujenga  tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kujiwekea mfumo bora wa maisha ili kuepukana na magonjwa sugu yasiyoambukiza.

Zoezi ambalo lilianzia mkoa wa Mara na kupata mwitiko mkubwa wa wakazi wa Mara kwa kupima watu 1582 na kufuatiwa na mkoa wa Shinyanga hususani wilaya ya Kahama ambako walijitokeza watu 700 linaendelea mkoa wa Geita , kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi ya Kalangalala, kuanzia tarehe 09/06/2014,  kwa siku mbili mfululizo, kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja Jioni.  Kambi hizi zinatarajia kuishia  katika  Mkoa wa Kagera.

HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA
Huduma mbalimbali zitatolewa  kwenye kambi hizi zikiwemo;
·         Upimaji wa Shinikizo la damu
·         Upimaji wa sukari kwenye damu- Kisukari
·         Upimaji wa hali ya lishe (Uwiano wa Urefu kwa Unene)
·         Utoaji wa dawa za Minyoo
·         Ushauri wa kitaalam kwa watakaokutwa na Matatizo
·         Ushauri nasaha  na upimaji hiari wa VVU (UKIMWI)
·         Kutoa vipeperushi vya Maelezo ya uboreshaji wa Afya.

Huduma  zote hizi zitatolewa na NSSF, BURE.

Pia kulikuwa na zoezi la uchangiaji wa damu kwa hiyari kwenye Benki ya Damu ya Mkoa ambapo Uniti za Ujazo 50 Ziliweza kukusanywa.

NSSF inaendelea kuwasii na kuwahimiza wakazi wa kanda ya ziwa kuwa waendelee kujiandikisha kwenye NSSF HIARI Scheme. NSSF HIARI Scheme ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo, wachimbaji wadogo, Ushirika wa Bodaboda , Ushirika wa Wakulima pamoja na wanachama wa Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii.

Jiunge na NSSF HIARI Scheme ili uweze kujipatia mafao bora ya NSSF yakiwemo Bima ya Afya BURE kwa familia nzima (SHIB), mikopo nafuu ya SACCOS,  pamoja na Mafao bora mengineyo.

Wananchi wa kanda ya ziwa wanakumbushwa na kuhimizwa kujitokeza kwa wingi ili kupimwa na kupewa ushauri wa afya zao Bure.

NSSF INAJENGA MAISHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE.
Kaimu Meneja wa Mafao ya Matibabu Dk. Lucy Simbila akizungumza kabla ya Kumkaribisha Mgeni Rasmi Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Geita Dk. Ndinisyu Daniel (kushoto) kufungua zoezi hilo. Wengine ni Dr. Ali Mzige (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Bw.Shaban Mpendu, Meneja wa NSSF Mkoa wa Geita na Mwisho ni Regional Aids Control Cordinator (RACC), Elisande Shumbi.
wakazi wa Geita wakiwa wamejitokeza kwa wingi kupima Afya zao.
Meneja wa NSSF GEITA, Bw. Shaban Mpendu akimsikiliza kwa makini  Dr. All MZIGE akimuelezea  mgeni rasmi kaimu mganga mkuu wa Geita   DR.Ndinsyu Daniel zoezi la upimaji sukari kwenye moja ya banda la upimaji afya.
Meneja NSSF Geita bwana Shaban Mpendu akimuongoza mgeni Rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa Geita  DR. Ndinisyu Daniel kutembelea mabanda ya upimaji afya.
Afisa Mwandamizi  Uendeshaji   Bi.Siaeli akiandikisha wanachama wapya waliojitokeza kujiandikisha kwenye kambi ya upimaji Afya.
Mmoja ya watu waliojitolea kutoa damu kwa hiyari baada ya kupima Afya kwenye kambi hiyo ya upimaji Afya
Mmoja wa Madaktari akimpima mkazi wa Geita Urefu na Uzito ili kutambua uwiano wa urefu kwa uzito na kujua hali ya kiafya (BMI)

No comments:

Post a Comment

Pages