Wanachama wakipata huduma kwenye banda la NSSF.
Ofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii (NSSF), Chiku Said akiwasikiliza wateja waliofika katika banda la NSSF kwa ajili ya kupata elimu na uandikishwaji. Kwa sasa shirika lina aina mbili ya uachama yaani wanachama wa hiari na ule wa kawaida. Katika kuhakikisha shirika linapanua huduma zake za hifadhi ya jamii ya watanzania wengi, NSSF imekuja na mpango maalum wa kuandikisha na kukusanya michango kwa wakulima , wajasiriamali, wachimbaji madini wadogo na wafanyabiashara ndogondogo.
Ofisa Mwandamizi Uhusiano na Huduma kwa Wateja
wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Theopista
Muheta (kushoto), akitoa maelezo kwa vijana waliotembelea banda la NSSF kwenye
maonesho ya pili ya biashara ya kimataifa yaliyoendelea katika viwanja vya
Tangamano mkoani Tanga.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Tanga, Frank Maduga (wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Kolla Prieto Hotel, Mr Muzamil kalokola (wa kwanza kushoto) na mbunge wa tanga mjini, Mtei Omar Nundu (katika), muda mfupi baada ya kupata maelo ya kazi za NSSF ambapo mwaka huu imezindua huduma mpya ya kuwafikia wachimbaji madini na wakulima na sek binafsi nyingine ili kuweza kuwafikia watanzania wote kwenye mfuko wa pensheni wa NSSF na kunufaika na mafao ya muda mfpi na muda mrefu. (Na Mpiga Picha Wetu)
Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma
kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume
(kushoto), akifurahia jambo na Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006),
Absalom Kibanda wakati alipotembelea banda la NSSF kwenye maonesho ya pili ya
biashara ya kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akitoa maelezo kwa wanachama alipotembelea kwenye banda hilo wakati wa maonesho ya pili ya kimataifa ya Biashara yaliyofanyika mkoani Tanga.
Kaimu Meneja wa NSSF Mkoa wa Tanga, Emmanuel Masika (kulia), akimsaidia mteja kujaza fomu za uanachama kwenye maonesho ya ya biashara ya kimataifa yanayofanyika mkoani Tanga, kwenye maonesho hayo NSSF imeluwa ikitoa elimu kwa Umma juu ya huduma zake na kuandikisha, kunadili kadi za zamani na zilizopotea, kutoa kumbukumbu za hesabu za wanachama na jushauri wa kiafya kwa wanachama wakewote wanaotembelea banda hilo.
Kaimu Meneja wa NSSF Mkoa wa Tanga, Emmanuel Masika (kulia), akimsaidia mteja kujaza fomu za uanachama kwenye maonesho ya ya biashara ya kimataifa yanayofanyika mkoani Tanga, kwenye maonesho hayo NSSF imeluwa ikitoa elimu kwa Umma juu ya huduma zake na kuandikisha, kunadili kadi za zamani na zilizopotea, kutoa kumbukumbu za hesabu za wanachama na jushauri wa kiafya kwa wanachama wakewote wanaotembelea banda hilo.
No comments:
Post a Comment