Kikosi cha Coastal Union |
Akizungumza leo Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema maandalizi ya
kuelekea mchezo huo yamekamilika kwa
asilimia kubwa na kinachosubiriwa na mechi hiyo itakayoanza saa kumi jioni
kwenye uwanja huo.
El
Siagi amesema baada ya kumaliza mechi hiyo timu hiyo itaelekeza mipango yake ya
kucheza mechi za kirafiki nyengine ili kuweza kujiweka imara kwa ajili ya
maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Amesema
wachezaji wa timu hiyo wataingia kwenye mechi hiyo kwa malengo ya kupata
ushindi ili kuweza kuendeleza rekodi ya kuwafunga wanakumanumanu hao ambao
msimu ujao watashiriki michuano ya ligi daraja la kwanza.
Kwa
upande wake,Ofisa Habari wa timu ya African Sports,Wanakimanumanu”Said
Karsandas amesema kuwa wamepania kushinda kwenye mechi hiyo ili kuweza
kurudisha ile heshima ya timu hiyo kwa wagosi hao wa kaya.
“Tunajua mechi hii itakuwa ni ngumu kutokana
na uwezo wa Coastal Union hivyo nasi tumejipanga kuweza kufanya vizuri ili
kutoa burudani kabambe “Alisema Karsandas.
Hata
hivyo aliwataka wakazi wa mkoa wa Tanga na viunga vyake kujitokeza kwa wingi
kushuhudia burudani itakayokuwa ikitolewa kwenye mechi hiyo .
Oscar Assenga .
Msemaji wa Coastal Union.
0714453839,Tanga.
No comments:
Post a Comment