NA
ELIZABETH JOHN
MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya nchini, Dudu Baya
amewataka wasanii wa muziki huo, Alikiba na Diamond Platinum kutumia vipaji
vyao kutengeneza hela na sio kugombana.
Kauli hiyo ya Dudu Baya imekuja baada ya wasanii
hao kuonekana wanaugomvi mkubwa ambao kila mmoja anauelezea kwa jinsi
anavyoujua.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Dudu Baya
alisema hao ni wasanii wenye vipaji na wanasoko kubwa katika tasnia hiyo hivyo
ni vizuri wakichukua nafasi hiyo kutengeneza hela na sio kugombana.
“Hawa ni wadogo zangu mimi nawashauri tu, wakae
chini wajitambue wao ni wakina nani wafikirie kutengeneza hela na sio kugombana
kila siku,” alisema.
Dudu Baya ni msanii ambaye alitamba kipindi cha
nyuma na ngoma yake ya ‘Nakupenda mpenzi’ ambayo ilifanya vizuri na kumtambulisha
vema katika soko la muziki huo.
No comments:
Post a Comment