HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 25, 2014

GSK YATANGAZA KUWASILISHA KWA CHANJO YA MALARIA

GSK imetangaza  kuwasilisha maombi ya udhibiti wa chanjo ya malaria RTS,S katika shirika ya  Ulaya ya Madawa Agency (EMA).
Uwasilishaji unafuata Ibara ya 58 ya utaratibu, ambayo inaruhusu EMA kutathmini ubora, usalama na ufanisi wa chanjo au dawa, zinazotengenezwa  viwandani vya nchi za  Umoja wa Ulaya (EU) kwa kutibu magonjwa yanayo tambuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kama magonjwa ya athari ya afya ya umma, lakini lengo kwa ajili tu ya matumizi nje  ya EU.

 Utathmini huu hufanywa na EMA kwa kushirikiana na WHO, na huhitaji madawa na chajo kufikia viwango vinavyokubalika kwa ajili ya matumizi katika nchi za  EU. Uhakiki kwa ajili ya maombi ulipewa na CHMP baada ya mkataba kutoka kwa WHO kuwa RTS, S kukamilisha vigezo kwa tathmini hiyo.
Matumizi ya RTS,S yamelengwa dhidi ya vimelea vya malaria vya Plasmodium falciparum, ambao vimenea zaidi katika bara la kusini mwa sahara Afrika. Makadirio yananoneyesha karibu asilimia 90 ya vifo kutokana na malaria hutokea katika bara la kusini mwa sahara Afrika , na asilimia 77 ya haya ni katika watoto chini ya miaka 5.
Uwasilishaji wa EMA ni hatua ya kwanza katika mchakato wa udhibiti kwa kufanya chanjo ya  RTS,S inapatikana kama mojawapo ya suluhisho za kuzuia malaria. 

Matumizi ya chanjo pamoja na suluhisho nyingine kama vile vyandarua na madawa ya kupambana na malaria huonyesha ukuaji wa mbinu za kudhibiti malaria. Hadi sasa hakuna chanjo yeyote ambayo imepata leseni ya matumizi kwa kuzuia malaria.

No comments:

Post a Comment

Pages