HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 10, 2014

Wakulima Momba waipa changamoto Serikali

Na Keneth Ngelesi, MOMBA

WAKULIMA wa Mahindi katika kijiji cha Isanga kata ya Nkangamo wilayani Momba Mkoani Mbeya wameiomba serikali kuweka  utaratibu kupanga bei elekezi ya pembejeo za kilimo ili kuwawezesha kujiwekea akiba katika kipindi cha mavuno ili utakapofika msimu wa kilimo waweze kumudu kununua pembejeo za kutosha kwa ajili ya mahitaji ya shamba.

Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na wakulima wadogo katika kikijiji hicho wakati wakijifunza mbinu za kilimo bora cha kisasa  kwenye shamba darasa la Dk. Samson Kibona ambaye amewekeza shamba lenye ukubwa wa hekta 70 za mahindi katika kijiji hicho.

Wakizungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti shambani hapo wakulima hao  walisema msimu wa kilimo, unapo fika  pembejeo za zimekuwa zikiuzwa kwa bei ghali wakati huohuo zingine zikiwa ni bandia, hali inayopelekea  kuathiri kwa kiasi kikubwa na kupata mavuno kidogo.

Miongoni mwa wakulima katika kijjiji hicho  Nanj Mwandandila alisema kuwa suala la upatikanaji wa pembejeo za kilimo hususani mbegu na mbolea ni changamoto kubwa kwa wakulima kutokana na bidhaa hizo kuuzwa kwa bei ghali.

Alisema kuwa wamekuwa wakiuziwa mbegu na mbolea kwa bei ghali na kwamba ni  changamoto kubwa inayopaswa kufanyiwa kazi na Serikali kwa kutoa bei elekezi ili kuepesha wakulima kupata hasara.

Naye Mercy Mwakyusa amabaye ni Mkulima na mfanyakazi katika shamba la Dkt Kibona alisema kuwa jambo baya zaidi linalopaswa kufanyiwa kazi kwa haraka na Serikali ni kudhibiti mbolea na mbegu feki wanazouziwa wakulima, kwa sababu tatizo hilo lina madhara makubwa wa kulima.

“Una jua la kuuziwa pembejeo feki ni baya zaidi, kwa sababu ukipanda mbegu zisipoota, unakuwa umepoteza muda na fedha na huwezi kupanda tena kwa sababu msimu umepita, lakini pia mbolea feki inasababisha mimeo kuharibika’ alisema Mwakyusa
Kwa upande wake Dk. Samson kibona alisema kuwa wakulima wadogo wa eneo hilo na maeneo mengine nchini wanahitaji kusaidiwa kupata zana za kisasa za kilimo ili waweze kuendeleza kilimo kwa kutumia teknolojia mpya.

Alisema kuwa kwa kuwaacha wakulima wenyewe wajinunulie zana za kilimo ambazo zinauzwa nchini kwa bei ghali, sio suluhisho la matatito ya wakulima, na badala yake akataka wakulima waungane na kuagiza zana za kisasa nje ya nchi wao wenyewe kwa gharama nafuu.

Kibona alisema Mkulima kutoa zaidi ya shilingi milioni 60 kwa wahindi wanapewa trekta moja na plau moja, na kwamba wakulima hao kufika hawawezi kumudi na vema kuwasadia wakulima ili waungane waweze kuagiza contena la zana za kilimo kwa bei ndogo ili waweze kupiga hatua ili kupiga hatua na kuondokana na umasikini. 

Diwani wa kata ya Tunduma, Frank Mwakajoka ambaye alifika shambani hapo kwa lengo kujifunza kutoka kwa mtaalumu huyo wa tiba mabadala alisema kuwa pamoja na changamoto nyingine zinazowakabili wakulima, mazao yao hayana soko la uhakika, jambo ambalo alidai kuwa ndilo linalozaa matatizo mengine.

 “Serikali ndiyo yenye wajibu wa kuwatafutia wakulima soko, lakini kwa bahati mbaya wakati mwingine Serikali ndiyo inayo waumiza kwa kuwazuia wakulima kuuza mazao yao kwenye soko la nje hali ambayo imekuwa ikiathiri maendeleo ya wakulima’ alisema Mwakajoka.

Alisema kuwa  suluhisho la matatizo yote ya wakulima ni kuwapatia soko la uhakika na lenye bei nzuri kwani  wakitafutiwa soko na wakauza mazao yao kwa bei nzuri, watakuwa na uwezo wa kumudu wenyewe pembejeo.

No comments:

Post a Comment

Pages