HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 29, 2014

ZESCO KUTUMIA TEKNOLOJIA MPYA YA KUFANYA UKARABATI WA NJIA ZA UMEME BILA KUZIMA

Mkurugenzi wa Mc Donald Liveline Technology, Donald Mwakamele akishangilia ushindi baada ya kampuni yake kuibuka na ushindi katika Maonyesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Zambia kwa teknolojia ya kukarabati njia za umeme bila ya kuzima. Wengine wataalamu aliowafundisha teknolojia hiyo ambao wote ni wanawake.



Na Mwandishi wetu

Shirika la Umeme la zambia (zesco) limeanza kutumia teknolojia ya kufanya ukarabati wa njia za umeme bila kuzima baada ya wafanyakazi wake kuhitimu mafunzo yalkiyokuwa yakitolewa na mtaalamu kutoka Tanzania Donald Mwakamele.

Akizungumza mjini Ndola baada ya kumalizika kwa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Zambia, Meneja Ufundi wa Zesco, Yona Sichwale alisema imekuwa furaha kwa shirika hilo kwani teknolojia hiyo itasaidia kupunguza gharama kwa shirika na pia usumbufu uliokuwa ukiwapata wateja pindi umeme ukizimwa.

"Tunashukuru kwa kupata teknolojia kutoka nchi jirani kwani Donald ametusaidia sana kwa kutufundishia kundi la kwanza la mafundi, tena wote wanawake".

Alisema mbali na teknolojia hiyo, lakini kikubwa ni kwamba Zambia inakuwa nchi ya kwanza kuwa na wataalamu wa teknolojia hiyo ambao ni wanawake watupu ambayo ni nadra sana kukuta duniani.

Alisema alistaabishwa jinsi watu walivyokuwa wanajaa katikas banda la Zesco nakushukudia wakinadada hao walkionyesha jinsi ya kufanya kazi bila kuzima umeme na kusababisha kutwaa ushindi katika sekta ya teknolojia, "Wazambia wengi hawakuamini kama inawezekana".

Menaja wa Zesco mkoa wa Copper belt Tom Daka alisema uamuzi wa kutumia teknolojia hiyo uliochukuliwa ni shirika lake ni sahihi kwani wamekuwa wakipata malalamiko ya mara kwa mara pindi umeme unapozimwa kwa ajili ya matengenezo.

"Itazuia hasara kwa shirika na hata wananchi kwani unapozima umeme shughuli nyingi zinakuwa hazifanyiki na hivyo kuwatia hasara wateja".

Mwakamele mwenyewe alisema kuwa amefarijika kuweza kufunduisha wanawake hao kwani watakuwa ndio genge pekee duniani linalofaya kazi kwa kutumia wanawake, "mara nyingi utakuta mwanamke mmoja kati ay wanaume kumi lakini sasa ni wenyewe tu".

Alisema kuwa baada ya mafanikio hayo ataendelea kufunduisha wengine nchini humo na katika nchi nyingine za Afrika ili teknolojia hiyo ienee kwani kwa sasa inatumika zaidi katika nchi zilizoendelea na baadhi katika Afrika Kaskazini na Kusini mwa Janga la sahara ni Afriak Kusini pekee.

No comments:

Post a Comment

Pages